Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde leo imetangaza kumwondolea wakfu wa Uaskofu aliyekuwa askofu wa Dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali.
Pia imeviondolea wakfu vifaa vya Kiaskofu alivyokuwa anatumia kama pete, msalaba pamoja na fimbo ambavyo alikabidhiwa tarehe 18 Januari 2018 alipowekwa wakfu kuiongoza Dayosisi ya Konde.
Uamuzi huo umefanyika leo Jumapili Juni 5, 2022 wakati wa lbada ya kumweka wakfu mrithi wake, Dk. Geofrey Mwakihaba.
Wamefikia hatua hiyo baada ya Dk. Mwaikali kugoma kuvirejesha ili vitumike kwa mrithi wake kwa mujibu wa taratibu za kanisa hilo.
Dk. Mwaikali aliondolewa madarakani tarehe 22 Machi 2022 na Mkutano Mkuu Maalum wa KKKT Dayosisi hiyo kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuiongoza vyema.
Vitu vingine ambavyo amegoma kuvirejesha ni kiti cha uaskofu na mavazi ambavyo navyo vimeondolewa wakfu.