Aliyekuwa Kocha wa Makipa Simba, Dan Cadena amwaga mboga Msimbazi, "wanaajiri wasio na weledi", alezea kipigo cha 5-1

Aliyekuwa Kocha wa Makipa Simba, Dan Cadena amwaga mboga Msimbazi, "wanaajiri wasio na weledi", alezea kipigo cha 5-1

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
"Tatizo kubwa la Simba ni kuajiri watu wasio na weledi. Kama Simba SC wanataka kufanikiwa wanapaswa kuachana na watu wasio na weledi"

"Simba kwa sasa inahitaji 'PROFESSIONAL PEOPLE' watu wenye Ueledi, wasipewe nafasi kwa sababu wanajuana na watu au Sababu wanaijua Sana Simba bali wanahitaji watu wenye Ueledi na taaluma"

𝗧𝘂𝗹𝗶𝗸𝘂𝗻𝗷𝗮𝗻𝗮 𝗺𝗮𝘀𝗵𝗮𝘁𝗶 :
"Mimi na Video analyst tuliwahi kukunjana mashati, hata kwenye mchezo wa (FA) dhidi ya Mashujaa Mchezo ambao Simba alitolewa kwa mikwaju ya penati baada ya dakika tisini kuisha Kwa Sare nilimfuata Mwalimu mkuu Benchikha na kumwambia kuwa Mwalimu siwezi kukupa taarifa yeyote kuhusu mchezo huu sababu Mchambuzi wa Video hajanitumia taarifa yoyote"

𝗞𝘂𝗵𝘂𝘀𝘂 𝗱𝗲𝗿𝗯𝘆 :
"Siku mbili kabla ya mechi ya Derby ya Kariakoo nilishangaa tu naambiwa Aishi Manula yuko tayari kwa ajili ya mchezo. Nilishangaa kwa sababu huwa sio kawaida yake, huwa naulizwa kuhusu hali ya makipa wangu lakini haikuwa hivyo"

"Sikutaka kupingana na kocha mkuu kwa kuwa sipendi kubishana na kocha mkuu na namheshimu, lakini siku hiyo hiyo niliongea na Aishi kwa sababu nimemfundisha na nilijua hayuko tayari kwa mchezo huo, ningekuwa naruhusiwa kutoa ushauri wangu usingecheza keshokutwa".

©️ Daniel Cadena

Aliyekuwa kocha wa magolikipa Simba SC ambaye ameamua kuondoka Simba baada ya mkataba wake kuisha mwezi huu.

Chanzo: Rick Media Sports
 
Alichosema tumekisema Mara nyingi tofauti aliyesema safari hii ni mtu aliyekuwepo benchi la ufundi.
Mechi ya Simba na Kaizer Chief wachambuzi kabla ya mechi Hawa nawazungumzuia wachambuzi wakubwa Afrika Kaizer wanafunga kwa mipira mirefu ya counter attack.
Ajabu magoli yote tulifungwa vilevile hapo unajiuliza kazi ya video analysis ni nini.
Mechi na Janangy wawa inajulikana hawezi kucheza cross lakini tulifungwa goli tatu zinazofanana. Kabla ya mechi na yanga madhaifu yalikuwa yanaonekana lakini walishindwa kurekebishwa.
Huyu kakaa na Gomez, Pablo, Roberthino, Benchika wote wameondoka Ila yeye kabaki wakati yeye ndiye mhusika mkuu..
 
na wewe unaleta habari kama sio proffesional tena.
 
Ufalme wa makolo umefikia tamati, ni masikitiko makubwa sasa rasmi Simba ni underdog. Dizaini kama vile Azam wamechukua nafasi yao.
Msimbazi Kila mtu anasema anapoona yeye panavuja na kumbe jumba zima ni bovu limeanguka
Dua la kuku hili mtaishiwa kunyewa na Mwewe...
 
Huyo cadena ameongea ukweli mtupu. Nchi tunaleta kujuana hata sehemu pasipostahili kwa mfano miaka na miaka kocha msaidizi simba lazima awe matola!? Sasa mpaka unajiuliza ivi hamna mtu mwingine anaestahili hiyo nafasi zaidi ya matola.

Maana matola almost miaka kumi yupo simba japo anaingia na kutoka na ukichunguza kwa makini hiyo nafasi anayopewa si kwa sababu ya uwezo wake bali kwa kuwa yeye ni simba damu.
 
Back
Top Bottom