Uchaguzi 2020 Aliyekuwa Mbunge wa Mwibara, Mutamwega Mgaywa apitishwa na Chama cha Sauti ya Umma (SAU) kugombea Urais

Uchaguzi 2020 Aliyekuwa Mbunge wa Mwibara, Mutamwega Mgaywa apitishwa na Chama cha Sauti ya Umma (SAU) kugombea Urais

Sauti ya Umma

Member
Joined
Aug 26, 2010
Posts
39
Reaction score
21
Muta.jpeg

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mwibara kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005 Mheshimiwa MUTAMWEGA MGAYWA amepitishwa kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU) katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi octoba Mwaka huu. Mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika jumamosi tarehe 25/7/2020 kwa kauli moja umempitisha mwanasiasa huyo nguli ili kupeperusha bendera ya chama hicho.

Pia Mkutano mkuu wa Chama hicho umewapitisha Bi SATIA MUSA SEBWA kuwa mgombea MWAMBATA na Ndugu ISSA MOHAMED ZONGA kuwa mgombea uraisi Zanzibar.

Akitoa shukrani zake kwa wajumbe mara baada ya kupitishwa kuwania nafasi ya Uraisi MUTAMWEGA MGAYWA alisema chama cha SAU ndio chama Pekee mbadala chenye sera bora na endelevu kwa ajili ya kumkomboa mtanzania na kuleta maendeleo.

-----

CHAMA cha Sauti ya Umma (Sau) nchini Tanzania, kimewapitisha wagombea wa urais wa Tanzania na Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkutano Mkuu wa chama hicho umefanyika leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020 jijini Dar es Salaam ambapo Muttamwega Mgaywa amepitishwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea mwenza atakuwa, Satia Musa Sebwa huku mgombea urais wa Zanzibar ni Issa Mohamed Nzonga.
Katibu Mkuu wa SAU, Majalio Kyara amesema, wagombea hao wamepigiwa kura kupitia mkutano mkuu wa chama baada ya kamati kuu ya chama hicho kuwajadili na kuyapendekeza majina mawili yapelekwe kwenye mkutano mkuu ili wapigiwe kura

“Awali, waliotia nia ya kugombea nafasi ya urais upande wa Tanzania majina yalikuwa matano lakini waliochukua fomu na kurudisha walikuwa wawili nikiwemo mimi (Kyara) pamoja na Mgaywa lakini niliamia kujiondoa ili aendelee na mchakato huu,” Kyara amesema.

Mara baada ya kutangazwa kuwa mgombea, Mgaywa amesema, nia yake ni kukijenga chama na siyo kuwa mpinzani wa maendeleo ambapo mawazo yao kwenda Ikuru.

Amesema, anataka kuijenga SAU kiwe chama cha kuleta maendeleo kama anavyofanya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli alivyoiletea nchi maendeleo.

Kwa upande wake, Nzonga amesema, anagombea nafasi hiyo kwa mara ya pili kupitia chama hicho hivyo aliwaomba wananchi watakapomchagua atafuata nyendo za Rais Magufuli kwa kuwa anafanya vizuri katika maendeleo.

“Tumeona Zanzibar Rais wa awamu ya saba na Rais Magufuli wamefanya vizuri katika maendeleo hivyo na mimi nitafuata nyendo zao,” amesema

Awali, Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza alisema alihudhuria mkutano huo kuangalia uchaguzi wa wagombea ambao umekwenda vizuri.

Amesema suala la rushwa likisimamiwa vizuri na vyama husika kwenye mchakato wa nafasi za ubunge, udiwani na urais watakaoenda tofauti wawachukulie hatua.

Uchaguzi Mkuu 2020: SAU yapata wagombea urais Tanzania, Z’bar
 
Hawa watu design hii siku siku NEC ikipiga panga hela za kampeni watapotea jumla
 
Back
Top Bottom