BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Eliud Jones Kijalo aliyekuwa Mhasibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Utalii ambaye amefunguliwa mashtaka hayo pamoja na mengine ya Kughushi, Matumizi Mabaya ya Mamlaka, Ufujaji na Ubadhirifu wa Fedha ulioisababishia hasara ya Tsh. Bilioni 4.03.
Mahakama imeelezwa kuwa kati ya Julai Mosi, 2016 na Julai 30, 2019 mshtakiwa akiwa katika ofisi za Wizara ya Maliasili iliyopo Temeke, aligushi vocha mbalimbali zenye thamani ya Sh 4,036,770,339 huku akijua ni kosa la kisheria.
Shauri hilo la Uhujumu Uchumi limefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar. Mshatakiwa alitakiwa kutojibu chochote kwakuwa Mahakama haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na amepelekwa mahabusu hadi Juni 28, 2023 shauri litakapotajwa tena.