Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha (Dkt. Pima) afunguliwa kesi mpya 2 za Uhujumu Uchumi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Your browser is not able to display this video.
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP, amemfutia Kesi na kumfungulia mpya mbili za Uhujumu Uchumia aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. John Marko Pima na wenzake watatu.

Kesi hizo zimefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha zikimkabili na wenzake watatu.

Kesi hizo zina mashtaka nane kila moja ikiwemo ya Ufujaji na Ubadhirifu wa Milioni 65 Fedha za Serikali.

Katika maelezo ya Kesi inadaiwa walijipatia kiasi hicho kwa kutumia Nyaraka kumdanganya mwajiri kuwa wamezitumia pesa hizo kumwaga moramu katika masoko ya Kilombero, Soko Kuu, Mbauda na Morombo, jambo ambalo sio kweli.

Washtakiwa wote wamekana mashtaka huku watatu wakiachiwa kwa dhamana.

Wasafi TV
Pia soma:


=====
Visa vya watu maarufu wengine waliowahi kutuhumiwa au kukamatwa na madawa ya kulevya
 
Shamba la bibi. Yote haya walifanya kipindi cha Jiwe
 
Kumbe makosa ya uhujumu uchumi yana dhamana
 
Si walishinda hii kesi wakaachiwa huru, wamefunguliwa tena[emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…