JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Evelyne na wenzake wamejiunga leo Septemba 8, 2024, kwenye mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Ilala uliofanyika Pugu, Dar es Salaam.
Ameeleza kuwa walichagua kuondoka Chadema na kujiunga na CCM kutokana na usikivu wa Rais Samia Suluhu Hassan, na maendeleo yanayoletwa na CCM katika sekta kama utalii, afya na miundombinu.
Everlyne amebainisha kuwa hayo ni miongoni mwa sababu kuu zilizowavutia kujiunga na chama tawala.
Akizungumza wakati wa kuwapokea, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga amesema kwamba Evelyne na wenzake wamefanya uamuzi sahihi kwa kujiunga na chama hicho wakati muafaka, kwani kinahitaji nguvu kazi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu amewapongeza kwa kuamua kujiunga na CCM.
Chanzo: Mwananchi