The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Wakuu vipi huko kwenu kampeni zinakwendaje
===
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilalanguru, Jimbo la Kigoma Kusini, mkoani Kigoma kwa tiketi ya CCM, Venance Chamaheke amemuombea kura mgombea wa ACT Wazalendo wa nafasi hiyo Juma Helandogo akieleza kuwa mgombea wa ACT anapaswa kufuata nyayo zake kwa kuendeleza alipoishia, na kuongeza maendeleo pale penye haja ya kuendelea zaidi.
Tukio hilo limetokea Novemba 21, 2024 wakati wa mkutano wa kampeni ACT Wazalendo katika kijiji hicho ambapo Venance amesema katika kipindi cha uongozi wake alifanya jitihada mbalimbali ikiwamo kutatua migogoro baina ya wakulima na wafugaji na ujenzi wa baadhi ya madarasa ya shule kijijini hapo, hivyo Helandogo anatakiwa kusimama kidete kuhakikisha maendeleo chanya zaidi yanapatikana ndani ya kijiji hicho.
Chanzo: Jambo TV