Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara kuteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa ni sawa?

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
1,281
Reaction score
1,251
Rais Samia amemteua ndugu Rodrick Mpogolo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu BARA WA CCM kuwa Katibu Tawala mkoa wa Katavi, hii imekaaje?

Kiongozi wa Kisiasa kupewa nafasi ya uongozi wa kiutawala Serikalini tena ni Technical post. Mhhh, nimeshangazwa Kama ilivyo kwa wanajeshi wasio wastaafu kupewa ukuu wa mkoa na Baadaye kurudishwa JESHINI, naona haiko sawa.

Mwaonaje wadau?
 
Shida ni nini kwani?
 
Tutashuhudia mengi ya kushtukizwa
 
Mama afanye afanyanvyo sisi tunataka hela mtaani tu,hata akimchagua Kingwendu haina shida.
 
Kila kitu kinawezekana.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar bwana Jecha alichukua form za kugombea Urais Zanzibar kupitia CCM.

Aliyewahi kuwa Jaji Mkuu Tanzania bwana Augustino Ramadhani alichukua form kugombea Urais kupitia CCM
 
Ndio mmetoka usingizini baada ya 17/3/2021
 
Tukio la mtanzania Mbunge kupigwa risasi mchana kweupe tena eneo linalolindwa maaskari ndio tukio la kushangaza zaidi tangu kuanza kwa jamhuri hii!!Hayo mengine hayana haja ya kushangaa ndugu yangu!!!
 
Tukio la mtanzania Mbunge kupigwa risasi mchana kweupe tena eneo linalolindwa maaskari ndio tukio la kushangaza zaidi tangu kuanza kwa jamhuri hii!!Hayo mengine hayana haja ya kushangaa ndugu yangu!!!
Ova.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…