Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Aliyekuwa ofisa wa Magereza, Josephat Mkama na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa manne likiwamo la kughushi msamaha wa Rais kwa wafungwa.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sibuti Nyabuya na Joseph Mpangala.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu Anna Magutu imetajwa mahakamani hapo leo Alhamisi Septemba 19, 2024.
Upande wa mashtaka umeieleza Mahakama kuwa umekamilisha upelelezi wa kesi hiyo.
Mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali, Winiwa Kasala ameiomba Mahakama ipange tarehe ya usikilizwaji wa awali ili washtakiwa wasomewe maelezo ya kesi.
Hakimu Magutu amekubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 26, 2024 kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.
Hakimu Magutu amewapa washtakiwa masharti ya dhamana likiwemo kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya Taifa ambao watawasilisha mahakamani fedha taslimu au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh7.5 milioni. Walishindwa kukamilisha masharti ya dhamana.