Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda ameachiwa huru baada ya kushinda kesi aliyokuwa akituhumiwa ya kumlawiti Mwanafunzi wa Chuo iliyokuwa ikieneshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi.
Dkt. Nawanda alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 9, 2024 na kusomewa shitaka moja la kulawiti kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16.
Akizungumza na Wanahabari baada ya hukumu hiyo, Nawanda amesema "Namuachia Mungu." kisha akaondoka eneo la Mahakamani.
Awali, kabla ya ushahidi wa upande wa mshtakiwa kuanza kutolewa, Julai 16, 2024 mbele ya Hakimu Marley, mashahidi wawili wa Jamhuri ambao ni Mwanafunzi anayedaiwa kulawitiwa pamoja na mama mzazi wa mwanafunzi huyo walifungua ukurasa wa kutoa ushahidi ambapo waliutoa kwa siri (faragha).
Pia, Soma: Hukumu ya aliyekuwa RC Simiyu, anayetuhumiwa kulawiti kutolewa leo Novemba 29