Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Mwanaume mmoja ameshtakiwa kwa kukwepa kupanga mstari wakati waombolezaji wakipita kwenye jeneza kuaga mwili wa Malkia Elizabeth II.
Mwanaume huyo ambaye anatoka Tower Hamlets mashariki mwa London, Muhammad Khan anadaiwa kupita nje ya foleni Ijumaa Septemba 16, 2022 na alikamatwa siku hiyo hiyo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vy kimataifa, urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya maombolezo kutoka katika Ukumbi wa Westminster yalikatwa wakati tukio lilipotokea.
Taarifa kutoka kwa Polisi imesema kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 alishitakiwa jana Jumamosi na atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Westminster kesho Jumatatu.
Kijana huyo amekuwa mtu wa pili kushtakiwa kwa kutenda kosa akiwa kwenye foleni ya kuuaga mwili wa Malkia II.
Mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 19 alishtakiwa baada ya kudaiwa kuvua nguo na kujaribu kuwanyanyasa kingono waombolezaji wa kike walipokuwa wakisubiri kwenye foleni katika bustani ya Victoria Tower Jumatano.
Kijana huyo Adio Adeshine alishtakiwa kwa makosa mawili ya unyanyasaji wa kijinsia na makosa mawili ya kukiuka amri ya kuzuia madhara ya kingono.
Mazishi ya kitaifa ya Malkia Elizabeth II yatafanyika kesho Jumatatu Westminster Abbey, London, kabla ya mwili wake kulazwa kwenye kasri la Windsor.
Kiongozi huyo wa kimila alifariki Alhamisi, Septemba 8, 2022 akiwa na miaka 96 huku akishikilia rekodi ya kuliongoza Taifa hilo kwa muda wa miongo saba.
Elizabeth alianza kuliongoza taifa hilo akiwa na miaka 25 tu mwaka 1952.
Mwananchi