Tetesi: Aliyemuua Mwangosi rufaa yake Wiki hii!!

Tetesi: Aliyemuua Mwangosi rufaa yake Wiki hii!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Habari toka kwa watu wa karibu wenye ufahamu na suala hili, wanasema kuwa aliyekuwa Askari Polisi na kutiwa hatiani kwa mauaji ya Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi, amekata rufaa na rufaa yake itaanza kusikilizwa siku ya Ijumaa ya tarehe 1/06/2018.

Pacifius Simon aliyekuwa Askari wa Kikosi cha kuzuia ghasia Mkoani Iringa, alihukumiwa kifungo cha miaka 15 Jela na Mahakama Kuu Kanda ya Iringa amekata rufani dhidi ya hukumu hiyo.
 
Watu jasiri yani umeua mtu na bado wakata rufaa uachwe huru, damu ya mtu haiendi bure atakwama tu.
 
upload_2018-5-29_14-9-11.jpeg

Mtuhumiwa Pacifius, kwenye maelezo yake ya kujitetea na picha ni tofauti kabisa! Eti anajitetea kuwa alishtukia tu mlipuko baada ya marehemu kumshika mkono! Stupid kabisa!
 
Atakuwa huru soon aungane na askari mwenzie aliye chomoa roho ya Akwilina......tahadhari awamu hii roho nyingi zitavunwa na Magufuli kupitia polisi au kundi lake la wasio julikana. kuweni makini!
Teh unatoa tahadhari halafu tena unajikaanga na mafuta yako
 
Wakati huyo askari mdogo akitumikia kifungo,maafisa wa juu walipandishwa vyeo,akiwemo Kamuhanda
....Anayekamatwa na ngozi ndiye mwizi wa mbuzi, hili liwe fundisho kwa hawa askari wadogo kwamba kama wanategemea wakifanya mauwaji kwa lengo la kufurahisha wakubwa mambo yakiwa mazito wanarukwa tuu na kutolewa kafara.
 
Mahakama itatenda haki, huenda akarudi uraiani kujumuika na familia yake
Mahakama ilishatenda haki ndo maana akahukumiwa. Hopefully Mahakama ya rufaa nayo itatenda haki na kuitupilia mbali rufaa yake ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Kwa awamu hii mbn ataachiwa tu km wale walopiga risasi za kukata kona
 
Aiseee auliwe na yeye kwel unampiga risas binadam mwenzako ... Sio risas Bomu !!! Aaaah ....
 
Back
Top Bottom