Aliyeniloga aah,Mungu anamuona.

Aliyeniloga aah,Mungu anamuona.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
ULIYENIROGA AA!

Mgunda naliandaa, mkulima najituma,
Naw'usisha Ulamaa, nipe mbinu za kulima,
Kisha nilipe jamaa, anipandie sukuma,
Mwisho napigwa butwaa, mazao yanachutama.

Mbegu toka manispaa, kweli nakula kasama,
Namwaga maji angaa, jua lisije kuchoma,
Usiku nawasha taa, kina tembo nawafuma,
Kesho dudu wamejaa, hapo licha ya huduma.

Niombeni ijumaa, Isilamu kila juma,
Niwasheni mshumaa, mungu anipe hekima,
Liniondoke kichaa, kwangu litendeke jema,
Jua huonyesha saa, ndoto iliyofuchama.

Najenga nyumba nakaa, niuache ukulima,
Bora kuuza makaa, mvua imesimama,
Shamba lilivyochakaa, mbele naona mlima,
Vipi ningegaagaa, upwa hautoki nyama.

Enyi mlionivyaa, mziwanda nala chuma,
Kutwa kucha najikwaa, na'mini sina karama,
Mzawenu sijang'aa, ndo sababu nalalama,
Wamiliki motokaa, na huku mimi kilema.

Uliyeniroga aa!, Wingu linaniandama,
Ninakupa makataa, sina tena uhalima,
Hainikuti fajaa, ingawaje waloloma,
Yupi atayenifaa, milele mpaka kiyama.

Uledi Bryan Rop
Kinda mtunga nudhumu
Nakuru KENYA
bryanrop8@gmail.com
+254724845351
27/11/2018_7:05 jioni
 
Back
Top Bottom