Aliyeomba rushwa ya Sh50,000 akwepa kifungo kwa kulipa faini ya Sh1 milioni

Aliyeomba rushwa ya Sh50,000 akwepa kifungo kwa kulipa faini ya Sh1 milioni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Ofisa mtendaji wa kijiji cha Ndedo kata ya Makame Wilayani Kiteto Mkoa wa Manyara, Yusuf Mrisho amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Sh50,000.

Hata hivyo, ofisa mtendaji huyo alilipa faini hiyo na kukwepa kifungo hicho.

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Kiteto, Mossy Sasi ametoa hukumu hiyo jana Ijumaa Machi 12, 2021.

Amesema Mrisho ametiwa hatiani kwa makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh50,000 kinyume na kifungu cha 15 (1) kikisomwa na 15 (2) vya sheria ya kuzuia rushwa namba 11/2007 .

Amesema mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka wa makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa, ambapo kwa kila kosa faini ni Sh500,000 au kifungo cha miaka mitatu jela.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Manyara, Holle Makungu amesema awali ofisi yao ya Kiteto ilipokea taarifa ya rushwa ya kikundi cha Upendo cha Ndedo.

Makungu amesema Mrisho aliomba rushwa ya Sh50,000 kwa kikundi cha Upendo ili awaandikie barua ya kufufua akaunti yao ya benki ambayo ilikuwa imelala.


MWANANCHI
 
hapo Mtendaji kaingia cha kike....🤣🤣🤣🤣🤣🤣
wacha wamnyoooshe.. Hao wanaupendo kazi hajafukuzwa huyo???????
 
Hapa sasa sheria ndio nimeielewa, uliiba 50 unalipa milioni sio yule anaekwapua bilioni mbili faini milioni 3.
 
Back
Top Bottom