Haya mambo yanahitaji uchunguzi, na subira, huyu naye chadema walisema katekwa na polisi
Your browser is not able to display this video.
=====
Jeshi la polisi mkoani Singida linawashikilia watu watatu akiwemo mganga wa kienyeji ambaye hajaweza kufahamika jina lake baada ya kutuhumiwa kumuua kijana samwaja na kumnyofoa baadhi ya viungo na kuufukia mwili wa kijana huyo katika makazi yake.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha makuro kata ya makuro tarafa ya mtinko halmashauri ya singida vijijin mkoan singida baada ya ndugu wa kijana samwaja na wananchi wa kata hiyo kumtafuta kijana huyo aliyepotea toka tarehe 8. 8.2024 wakati akitizama mechi ya ngao ya hisani kati ya Yanga na Simba.
Baadhi ya wananchi walianza kumtilia shaka mganga huyo wa kienyeji aliyehamia katika kijiji hicho hivi karibuni huku akiwa na matukio ya kuchinja mbuzi na ng’ombe za watu katika kijiji hicho licha ya wananchi hao kuripoti matukio hayo kwa viongozi.
Mkuu wa wilaya ya singida godwin gondwe amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akielezea hatua ambazo zimechukuliwa na serikali.
Wananchi wa kata hiyo wanaeleza kuwa kuna watu 3 ambao wamepotea katika mazingira ya kutatanishabkatika kata hiyo ambao bado hawajapatikana.
Duh kwahiyo huyo mganga ni jirani yako mkuu? Ni kweli alikuwa na hayo matukio ya kuchinja mifugo ya watu bila ruhusa? Na kwanini hawakumchukulia hatua kama hilo lilikuwa linatokea kitambo?
Upo hapo nyumbani na umethibitisha kwa macho yako baada ya mwili kufukuliwa au ni maneno tu ya kiufikishaji habari?
Ddduuuhhh bora sie wala urojo mdebwedo tukishashiba urojo wetu hatuna shida na mtu. Maisha gani hayo kila siku taarifa za watu kuuwana, tena kikatili...ndio kutafuta pesa kwa nguvu zote!!!?
Duh kwahiyo huyo mganga ni jirani yako mkuu? Ni kweli alikuwa na hayo matukio ya kuchinja mifugo ya watu bila ruhusa? Na kwanini hawakumchukulia hatua kama hilo lilikuwa linatokea kitambo?
Upo hapo nyumbani na umethibitisha kwa macho yako baada ya mwili kufukuliwa au ni maneno tu ya kiufikishaji habari?
Mimi nipo mkoa mwingine kimakazi ila mahali tukio limetokea ni jirani na home kwetu kabisaa hata familia ya kijana iliodhurika naifahamu na kijana namfahamu ila hayo mengine sijui