ALIYESABABISHA MSIBA NA KILIO,GHAFLA ANAGEUKA KUWA MFARIJI.

ALIYESABABISHA MSIBA NA KILIO,GHAFLA ANAGEUKA KUWA MFARIJI.

Jamiitrailer

Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
80
Reaction score
208
Hii ni ajabu na kweli,na inatokea Tanzania tu. Serikali ndiyo iliyotangaza kufutwa kwa vijiji na kuamuru watu waondoke eneo la Ngorongoro. Lakini baada ya malalamiko toka kwa waathirika na watu wengine, serikali hiyo hiyo kupitia watendaji wake waliomiminika eneo hilo na kutoa maneno ya faraja kwa walalamikaji kiasi cha kukufanya uamini kwamba waliotoa amri ya kuwaondoa watu ni serikali ya nchi nyingine.

NB: Ushauri wa bure kwa serikali: Kama kuwamisha wamasai Ngorongoro ni suala lenye tija,namna pekee ya kuwaondoa ni kuwashirikisha kwa kuwaelimisha kwanza viongozi wa jamii yao,Laigwanan..,kisha hao malaigwan ndo wawaelimishe watu wao kwa nini serikali inaona ni muhimu wao wahame maeneo ya hifadhi. Na Wamasai wana mfumo wa kijamii wenye nidhamu..kamwe hawapingi viongozi wao wakishaelewa somo.
Ilichokosea serikali ni kutumia ubabe wa kishamba badala ya kuwalainisha wahusika kwa hoja.
 
Back
Top Bottom