Inawezekana vipi 'Wanamume' wameumia Darasani huko UDSM, SAUT na Mzumbe halafu Wewe uliyesoma OUT ( hapo Biafra ) na Kupata Degree ( Shahada ) yako tukikutana Vijiweni uwe na la Kuchangia?
Elimu ya Masafa 'inamheshimisha' Mtu kweli au ndiyo labda 'inamdharaulisha' mbele ya wale Waliohudhuria 'Lecture Sessions' zote kwa miaka Mitatu au Minne na Kupata Bachelors zao walizozihangaikia Darasani huku 'sometimes' wakipata 'Sapu' za Kutosha tu.
Anaongea vizuri sana, tena anawatoa njeee!! Ukitaka kujua ubora wa elimu ya masafa ya OUT
1. Mitaala ya OUT inasimamiwa na TCU, kuhakikisha ubora unadhingatiwa! Mbona hakifutwi kama ni dhaifu?
2. Wakigraduate mfano LLB wanakwenda Law school na kukimbizana ipasavyo na hao wa conventional!
3. Wahasibu wanaomaliza mafunzo OUT wanapita bodi za uhasibu na kupata CPA na taaluma zinginezo.
4. Interview za serikali au binafsi mnachanganywa wote humo!! Mara nyingi walomaliza OUT hupata kushinda!! Hapo vipi??
5. Unajua kuna wanataaluma nguli wa hivyo vyuo ulivyotaja ambao ni zao la OUT?? Tena wanawafundisha nyie. Au niwataje??
6. OUT ni chuo bora kabisa kwa sasa ni namba moja barani Africa kwa vyuo vinavyotoa elimu masafa miongo mwa mlolongo wa vyuo kutoka mataifa bora kabisa kielimu. Hadi UNISA walikwenda OUT kujifunza??
7. OUT ndiyo taasisi namba moja kwa mwaka 2021 Tanzania kwa matumizi bora ya TEHAMA inayotolewa na tume ya TEHAMA nchini. Hapo UD tupa kule, SUA kanyaga, Mzumbe sogeza vile, tuzo alitoa Mh. Majaliwa huko Arusha.
8. Imepata Recognition certificate kutoka ATU, unawajua hao?? 🤣🤣🤣
Kwa vigezo hivyo, nakuhakikishia kabisa kuwa wanaume wanaomaliza OUT wanapaswa kuheshimiwa. Akisimama mnapaswa mkae chini kwa heshima!! Wenzenu wanapiga nondo kwa malengo na si michezo yenu ya kufuata wanafunzi wakike vyumbani mwao muwakulena kuwapa alama (refer mhadhiri wa UDOM).