Aliyetoka jela kwa msamaha wa Rais akamatwa kwa kufanya uhalifu kwa kutumia sare za JWTZ

Aliyetoka jela kwa msamaha wa Rais akamatwa kwa kufanya uhalifu kwa kutumia sare za JWTZ

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Jeshi la Polisi Kanda ya Dar linamshikikia Emmanuel Joseph Magoti kwa kukutwa na sare za JWTZ ambazo ni suruali 2, koti 1 na Tshirt 1.

Bw. Magoti ambaye alikamatwa maeneo ya Mbagala baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema na baadaye kukutwa na sare hizo nyumbani kwake, amekiri kutumia sare hizo kufanyia uhalifu akiwa na wenzake wawili ambao bado wanatafutwa.

Magoti alikuwa mfungwa katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam na aliachiwa kwa msamaha wa Rais mwaka 2018.

Kamanda Mambosasa ametoa onyo kwa wote wanaopewa msamaha kutoka gerezani wabadili tabia zao kwani lengo la msamaha ni kubadilika na si kuendelea na tabia za awali.

Tahadhari kwa wananchi kuhusu matapeli

Jeshi la Polisi kanda ya Dar pia imetoa tahadhari kwa wananchi kuhusu matapeli hasa kupitia mitandao ya simu.

Kamanda Mambosasa amesema hakuna mtandao unaofanya michezo ya kubahatisha unaotaka mshindi atoe pesa kwanza ili aandaliwe mazingira ya kupewa zawadi au ushindi wake.

Pia amewaasa wananchi kuepuka vitu vya bure kwa sababu wengine wanaambiwa wameshinda bahati nasibu ilhali hawakushiriki.

Kamanda ametoa pia namba za simu ambazo hutumiwa sana na matapeli hao ambazo ni 0758 713746, 0764 581220 na 0744 105579 na kusisitiza kuwa matapeli wanaweza kutumia namba yoyote.

Kamanda amemalizia kwa kutoa tahadhari kwa wanunuzi wa viwanja na magari hasa wanaotoka mkoani kuwa makini wanapofanya manunuzi hayo ili kuepuka kutapeliwa na wauzaji feki.
 
Jeshi la Polisi Kanda ya Dar linamshikikia Emmanuel Joseph Magoti kwa kukutwa na sare za JWTZ ambazo ni suruali 2, koti 1 na Tshirt 1.

Bw. Magoti ambaye alikamatwa maeneo ya Mbagala baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema na baadaye kukutwa na sare hizo nyumbani kwake, amekiri kutumia sare hizo kufanyia uhalifu akiwa na wenzake wawili ambao bado wanatafutwa.

Magoti alikuwa mfungwa katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam na aliachiwa kwa msamaha wa Rais mwaka 2018.

Kamanda Mambosasa ametoa onyo kwa wote wanaopewa msamaha kutoka gerezani wabadili tabia zao kwani lengo la msamaha ni kubadilika na si kuendelea na tabia za awali.
Ishu siyo kutoka, ishu ni atakula wapi? Sare ya jeshi ni ajira especially kwa mbumbumbu wa kwetu pazuri Mbagala
 
Back
Top Bottom