Pre GE2025 Aliyetuhumiwa kupanga kumfukuza John Mrema CHADEMA akanusha

Pre GE2025 Aliyetuhumiwa kupanga kumfukuza John Mrema CHADEMA akanusha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
CHADEMA wa Kata ya Segerea mkoani Dar es Salaam, Kitomary Steven, amekanusha vikali madai yaliyoenezwa mtandaoni kwamba amepanga kumvua uanachama John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA.

Akizungumza na Jambo TV, Kitomary ameeleza kuwa taarifa hizo ni za uongo na hazina msingi wowote.

“Ninaomba nikanushe taarifa hizo, taarifa hizo ni ghushi. Kwanza kabisa, mimi ni Mwenyekiti wa CHADEMA wa Kata ya Segerea, huku Mrema akiwa ni mkazi wa Kata ya Bonyokwa na Mkurugenzi wetu wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, ambaye tunamheshimu sana,” amesema Kitomary.

Pia, Soma: John Mrema: Wanataka kunifukuza uanachama. Wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme

Ameendelea kueleza kuwa haikubaliki kisheria wala kimantiki kwa ngazi ya tawi kufikia maamuzi ya kumvua uanachama Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ambaye pia ni sehemu ya Sekretarieti ya Makao Makuu.

Awali, John Mrema alitoa madai kupitia ukurasa wake wa X kwamba viongozi wa CHADEMA, akiwemo Kitomary, walikuwa wakipanga kumvua uanachama kabla ya mkutano wake na waandishi wa habari uliotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Katika ujumbe wake, Mrema aliandika: "Nimejulishwa na mwenyekiti wa tawi langu, ameagizwa anifute uanachama kabla ya kesho ili kama nitaendelea na nia yangu ya kuzungumza na vyombo vya habari basi niwe sio mwanachama!”,

Mrema aliongeza kuwa juhudi za kumvua uanachama ni sehemu ya juhudi za kuzima maoni huru na uhuru wa kujieleza ndani ya chama.

Kitomary amefafanua kuwa Mrema alichapisha ujumbe wa kuashiria kuwa angefanya mkutano na waandishi wa habari, ambapo Kitomary alijibu ‘tweet’ hiyo kwa kumweleza kuwa mkutano huo utafuatiliwa kwa ukaribu.

 
Ni kwanini John Mrema ana hofu na mashaka vile..?

Ana madhambi yanayomsuta mwenyewe nini kiasi cha kuanza kujishitukia na kujihami wakati hiohuo..?

Hii ni HEKIMA ya wapi ya kusema anaitisha Press Conference na kusema ya moyoni na kwa "mdomo mpana zaidi?"

Shida kubwa ya watu wa Freeman Mbowe (Team Mbowe) ni kukosa hekima ya kutambua nyakati na majira ya kufanya maamuzi fulani ikiwemo waseme nini, wakati gani, kwa nani na mahali gani..!

Huyu (John Mrema) naye ameikosa kabisa hekima hii...
 
Lakini Mwenyekiti mstahafu alionya hii tabia ya kuitisha mikutano
 
Huyu na Kigaila wana hofu zaidi naona hata Salum Mwalimu amekimbia kusema hataki unaibu katibu mkuu kumbe alishahisi mambo yamevurugwa.

Kigaila ndio hata hakuaga mkutano mkuu alikimbia tu baada ya kusikia Lissu anaongoza kura.

Sasa amefuata Mrema, anajishtukia nini? Asubiri Lissu "afike" ofisini ndio mengine yafuate.
 
Huyu na Kigaila wana hofu zaidi naona hata Salum Mwalimu amekimbia kusema hataki unaibu katibu mkuu kumbe alishahisi mambo yamevurugwa.

Kigaila ndio hata hakuaga mkutano mkuu alikimbia tu baada ya kusikia Lissu anaongoza kura.

Sasa amefuata Mrema, anajishtukia nini? Asubiri Lissu "afike" ofisini ndio mengine yafuate.
Lissu ni mhuni kama wahuni wengine.
 
Back
Top Bottom