CHADEMA wa Kata ya Segerea mkoani Dar es Salaam, Kitomary Steven, amekanusha vikali madai yaliyoenezwa mtandaoni kwamba amepanga kumvua uanachama John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA.
Akizungumza na Jambo TV, Kitomary ameeleza kuwa taarifa hizo ni za uongo na hazina msingi wowote.
“Ninaomba nikanushe taarifa hizo, taarifa hizo ni ghushi. Kwanza kabisa, mimi ni Mwenyekiti wa CHADEMA wa Kata ya Segerea, huku Mrema akiwa ni mkazi wa Kata ya Bonyokwa na Mkurugenzi wetu wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, ambaye tunamheshimu sana,” amesema Kitomary.
Ameendelea kueleza kuwa haikubaliki kisheria wala kimantiki kwa ngazi ya tawi kufikia maamuzi ya kumvua uanachama Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ambaye pia ni sehemu ya Sekretarieti ya Makao Makuu.
Awali, John Mrema alitoa madai kupitia ukurasa wake wa X kwamba viongozi wa CHADEMA, akiwemo Kitomary, walikuwa wakipanga kumvua uanachama kabla ya mkutano wake na waandishi wa habari uliotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Katika ujumbe wake, Mrema aliandika: "Nimejulishwa na mwenyekiti wa tawi langu, ameagizwa anifute uanachama kabla ya kesho ili kama nitaendelea na nia yangu ya kuzungumza na vyombo vya habari basi niwe sio mwanachama!”,
Mrema aliongeza kuwa juhudi za kumvua uanachama ni sehemu ya juhudi za kuzima maoni huru na uhuru wa kujieleza ndani ya chama.
Kitomary amefafanua kuwa Mrema alichapisha ujumbe wa kuashiria kuwa angefanya mkutano na waandishi wa habari, ambapo Kitomary alijibu ‘tweet’ hiyo kwa kumweleza kuwa mkutano huo utafuatiliwa kwa ukaribu.
Kazi kweli kweli. Bado Bon Yai, Ntobi, Benson Kigaira, na Yericko Nyerere nao kukimbilia tweeter kuomba huruma ya wanachama ili wasifukizwe kwenye chama, au kuondolewa kwenye nyazfa zao.
Ana madhambi yanayomsuta mwenyewe nini kiasi cha kuanza kujishitukia na kujihami wakati hiohuo..?
Hii ni HEKIMA ya wapi ya kusema anaitisha Press Conference na kusema ya moyoni na kwa "mdomo mpana zaidi?"
Shida kubwa ya watu wa Freeman Mbowe (Team Mbowe) ni kukosa hekima ya kutambua nyakati na majira ya kufanya maamuzi fulani ikiwemo waseme nini, wakati gani, kwa nani na mahali gani..!
Huyu (John Mrema) naye ameikosa kabisa hekima hii...
Kazi kweli kweli. Bado Bon Yai, Ntobi, Benson Kigaira, na Yericko Nyerere nao kukimbilia tweeter kuomba huruma ya wanachama ili wasifukizwe kwenye chama, au kuondolewa kwenye nyazfa zao.