Aliyetunga sheria/adhabu ya kuwanyonga Wakristo, ana IQ ndogo?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Ni ajabu hadi leo kuna nchi duniani ambazo bado zinatoa adhabu ya kumnyonga mtu aliyeamua kuacha dini yake ya mwanzo na kuwa Mkristo. Aliyebuni sheria/adhabu hiyo aliona kwamba hiyo ndiyo njia ya kuwakomesha wafuasi wa Kristo. Najiuliza: aliyetunga sheria/adhabu hiyo alishindwaje kuelewa Andiko hili rahisi kabisa kueleweka? “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa, atakuwa anaishi” (Yohana 11:25).

Mtu akifa katika Kristo, ni sawa na mtu aliyelala tu. Siku ya ujio wa Yesu, wote waliokufa katika Kristo watafufuliwa na kuungana na watakatifu watakaokuwa hai duniani, kisha Yesu atawanyakua na kuwapeleka mbinguni kwenye uzima na raha ya milele (1 Wathesalonike 4:16-17). Hivyo kifo cha Mkristo wa kweli, sio mwisho wa maisha, bali ni daraja la kuingia katika uzima wa milele na kushiriki ushindi wa Kristo juu ya dhambi na kifo.

Waliosoma historia wanakumbuka vizuri jinsi Mfalme Nero wa Roma alivyowatesa na kuwaua Wakristo kwa moto na kuwanyonga. Alidhani kwa njia hiyo, ataifuta kabisa imani ya Kikristo. Lakini badala yake, damu ya wafia imani ikawa mbegu ya kukua kwa Kanisa. Kadiri walivyouwawa ndivyo Injili ilivyoenea zaidi.

Ndivyo ilivyokuwa pia kwa waliomuua Yesu; walifikiri wamemkomesha. Lakini siku ya tatu alifufuka na Yuko hai sasa na hata milele. Amina
 
Really? Kuna nchi zinanyonga mtu aki-convert kuwa Mkristo?
 
Ila wewe umeandika utafikiri wanaouawa ni wale wanaokuwa wakristo tu wakati kiuhalisia ni kila dini
 
Sio ukristo tu ila kila dini
Kama umeisoma vizuri mada, imejikita zaidi kuelezea nchi zinazotekeleza sheria ya kuwanyonga wanaoamua kuacha dini zao za mwanzo na kuwa Wakristo
 
Ila wewe umeandika utafikiri wanaouawa ni wale wanaokuwa wakristo tu wakati kiuhalisia ni kila dini
Ushahidi nilio nao ni wa Wakristo tu. Wa dini nyingine sina
 
Kama umeisoma vizuri mada, imejikita zaidi kuelezea nchi zinazotekeleza sheria ya kuwanyonga wanaoamua kuacha dini zao za mwanzo na kuwa Wakristo
Nilijua uazungumzia nchi za kiislamu
 
Dini inayoamuru kuuwa mtu kwa sababu za kidini au Kisiasa na Kijamii, nina uhakika hiyo sio Dini ya Mungu Mwenyezi:
Yakobo1:26
Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.
27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Mungu ni upendo:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…