Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wakati mgogoro ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Konde ukifikia kwenye hatua ya kugombea mali, imefahamika kuwa hatimaye upande wa uongozi uliondolewa madakani umekubali kurejesha mali za kanisa hilo.
Mgogoro uliibuka baada ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Geofrey Mwakihaba huku aliyevuliwa Uaskofu na madaraka mengine yote Dkt. Edward Mwaikali ikidaiwa yeye na wanaomuunga mkono kugoma kurejesha mali za kanisa hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema: “Nimekutana na pande zote, uongozi wa sasa na ule wa zamani unaoongozwa na Dkt. Mwaikali ambaye amerithia mbele yangu kuwa atarejesha mali zote ikiwemo magari, zoezi hilo litaendelea hadi kufikia Juni 22, 2022 pia na yeye ameomba apatiwe stahiki zake.”