ana kesi ya kujibu na yeye......
ila mimi kwa kweli ntalia sana na mwanamke anayejua kabisa huyu ni mume wa mtu na bado anakosa heshima kiasi hicho. wengine huwa wandanganywa 'sijaoa'........huyo anagalau ana cha kujitetea. shemeji yangu aliwahi kumdanganya binti hajaoa, sisy alipogundua mumewe ana cheat alimpigia yule binti na binti akajieleza na that was it.....
alaaaa!! mume mtamu dearest huh!!! si unaona mi ndo mana nasema 'cheza na mimi' usicheze na 'mume wangu'............tena dharau zilizopitiliza kama hizo ........I would be too nice to her nimwache tu aende na kovu tu.
Linapokuja suala la mume au hata mke (kwa upande wetu wanaume) ni jambo gumu sana. Huwezi hata siku moja kujua uta-react vipi ukikutana na mauza uza ya namna yoyote. Hata hivyo unahitaji kumwomba Mungu kwani unaweza kukuta uamuzi uliouchukua unakutia mwenyewe matatizoni. Kuna wanawake ambao wamejikuta wakiambulia kichapo cha mbwa mwizi toka kwa waume zao wakisaidiana na hao hawara (kugombelezea) kwa kisingizio kuwa wameanzisha fujo. Kwa hiyo kabla ya kuanzisha kipigo ni muhimu kuangalia huyo mume atakaa upande gani.Au uwe tayari kuwapambana nao wote, na pia kumpoteza mume ikibidi.
Dada yangu ameachana na mume wake baada ya huyo mume kumsaidia hawara yake kumfungulia kesi mahakamani eti kwa kosa la kumgawia kichapo huyo hawara. Huwezi kuamini, huyo mwanamume ndiye alikuwa shahidi wa kwanza wa hawara yake. Ila baada ya dada kushinda kesi, mume wake alijaribu kuomba msamaha na dada akamwambia kuwa mke anayemtafuta yuko jela. Ndoa imekufa fa!!
je angeshindwa?.....hapo mbona hakuna cha kusamehewa jamani, yaani hatakiwi hata kuonekana mbele ya macho ya mkewe, ameendelea na hawara auahawara nae alimmwaga?(au hamjajua?)...hata mie hapo ndoa ingekufa kibudu.
Huyo mdogo wangu ana misimamo kama yako kiasi kwamba nampenda sana. Mimi nilikuwa namchukia sana huyo shemeji yetu basi tu. Nadhani hata angeshindwa kesi hiyo ndoa ilishakufa siku nyingi. Kwa sababu huyo mwanamume alikuwa kama shetani kabisa. Kuna wakati mke wake alipandwa na pressure hadi kulazwa hospitali ila nilipompigia simu kumuuliza kulikoni, akadai mke wake ni mwongo haumwi!
Dada alipata shinikizo la ndugu ili amsamehe mume wake lakini alikataa kata kata na sasa anaendesha maisha yake vizuri tu na ni mwaka wa 2 umepita. Jamaa ameoa mke mwingine tofauti na yule hawara yake na nadhani bado anaendelea na huo ukware wake. Hata hivyo mambo yake si mazuri kiasi kwamba bado anamuota mke wake wa zamani!
hapo mie ndipo ninapopapendaga, yaani mtu anatakiwa ajute milele, hee mdog wako nae alipata msukosuko eehh...hapo unakuta pressure imepanda kwaajili yake bado unaambiwa hayo...yaani game jamani ni gumu sana hili.
Hii ungeifanya signature yako kabisa...ingependeza sanaAziniye na mwanamke hana akili kabis; anafanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Nyamayao mbona hivyo .......... wenzio wale wapi ? :smile: ati wanasema tunabanana humuhumu ....... alafu mnasema wanaume walafi .........usijaribu, usijaribu.....amekosa kote huk anataka kujishikisha kwako, baadhi ya wanawake wanapenda kujipotezea muda kweli, mie nilivyo na wivu nikae na mtu nusu saa aniambie namuwahi mke wangu cjui kama ningeweza huo ulimwengu, ucmkubali...yaani sasa hivi ndio anakuona wa maana japo umeoa?
Mshkaji nenda msibani ........... huwa tunazika hata tusiowafahamu ....... TIP baba binti maringoKwa muda mrefu amekuwa kimya baada ya kumfungia vioo. Wiki iliyopita kaniandikia email baba yake mgonjwa nikamuone, sikwenda. Leo kanitumia email baba yake alifariki na shughuli za msiba zimeisha. Hakunitaarifu in time kwa sababu sikutaka kwenda kumuona baba yake wakati mgonjwa. Nimemjibu nimempa pole nikaahidi kupita kwao nikitoka kazini.
yaani hawa viumbe jamani, wakati mwingine unajiuliza aliolea nini kama bado alikuwa hajamliza mambo yake, sasa na wewe dada unadanganywa mtu hajaoa hata anapoishi hujui/hujauliza?....po mwaka mzima mnaishilia hotel huhoji anaishije?