Pre GE2025 Aliyewahi kuwa Mbunge wa Lupembe: Ubunge sio kujua kusoma na kuandika pekee. Ni lazima ujue Kiingereza na sheria. Kutunga sheria ni kazi ngumu

Pre GE2025 Aliyewahi kuwa Mbunge wa Lupembe: Ubunge sio kujua kusoma na kuandika pekee. Ni lazima ujue Kiingereza na sheria. Kutunga sheria ni kazi ngumu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Lupembe mkoani Njombe ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Njombe Jolam Hongoli amewataka Watanzania kuacha kufikiria kuwa ili uweze kuwa Mbunge unapaswa kujua kusoma na kuandika tu kwa kuwa kazi hiyo ya uwakilishi ni kubwa na inahitaji maarifa.

Hongoli ameeleza hayo wakati akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mavanga mara baada ya Jumuiya ya Wazazi kufika shuleni hapo na kupanda miti pamoja na kutoa elimu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM huku akiwataka wanafunzi kuongeza bidii kwenye masomo kwa kuwa serikali imeendelea kutekeleza Ilani kwa kujenga miundombinu ya kutosha.

"Chama Cha Mapinduzi kinataka watoto wote mfaulu kwasababu mtaweza kujiajiri au kuajiriwa, na kuna wengine wanasema ubunge ni mradi ujue kusoma na kuandika sio kweli, kazi ya mbunge ni kubwa kwa kuwa ni lazima ujue Kiingereza, sheria kidogo mambo ya elimu na mambo mengine kwa hiyo kutunga sheria ni kazi ngumu", amesema Hongoli.

Licha ya mambo mengi yaliyofanywa na Jumuiya katika kuchagiza kilele cha kuzaliwa kwa CCM lakini pia imefanikiwa kuwashika mkono kwa kuwawezesha vitu mbalimbali ikiwemo sukari na sabuni wazee ambao ni waasisi wa chama hicho wanaoishi kata ya Mavanga


Ubunge.png
 
Utadhani kuna mashindano ya kuanzisha nyuzi

Duh aiseee
 
Ni haki yake kusema yaliyo moyoni. Huenda walimzungusha ili asiweke mambo wazi.
 
Hebu awatafute wabunge, Msukuma na Kibajaji aongee nao. Waliingiaje bungeni? Cv yao ikoje?
 
Back
Top Bottom