KERO Aliyewapiga mkwara Dawasa Dar please tunaomba nenda Mwanza na mikoa mingine.Tumeona matunda within 24 hours

KERO Aliyewapiga mkwara Dawasa Dar please tunaomba nenda Mwanza na mikoa mingine.Tumeona matunda within 24 hours

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

the power

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
407
Reaction score
799
Hivi jamani, sisi wabongo watu wa ajabu sana? hivi ni kwa kuwa hatuelewi majukumu yetu?hivi ni kwa sababu sisi ni wavivu, hivi sisi hatujui kwa nini tumeshika ofisi zetu.hatujui wajibu wetu? Hivi ni mpaka mtu apigwe mkwara wa kufukuzwa kazi, aumbuliwe mbele ya ma-subordinates wake ndipo afanye kazi, atimize wajibu wake kwa kufanya kazi zake za msingi?Kama kazi zake za msingi hawezi,huyu kiongozi unategemea atakuwa proactive kucreate new development na kuwa creative?

Nimeona kwenye magroup ya mitandaoni Bosi wa wizara ya maji akimpiga operation manager wa Dar es Salaam Water and Sanitation Authority (DAWASA) mkwara mzito balaa na kumvua nguo jamaa. Kesi ni kwamba Bosi wa Dawasa anaandika reporti nzuri sana,report safi ya kila mwezi kuhusu operation za idara na upatikanaji wa maji.

Jamaa anareport kima cha maji Ruvu kiko sawa, jamaa anasema flow ya maji kwa Dar ni superb, matanki yote makubwa manane ya kuhifadhi maji Dar ni safi kabisaa, yaani yamejaa vizuri ,yote yamefurika na yanatiririsha maji murua kabisa bila shida yeyote.

Kwa kweli sisi wa Dar es salaam, kinondoni, ilala, sinza kote huko na maeneo ya ubungo na kwingine labda tuwaambie ukweli tulishaanza kusahau maji ya 24 hours ,maji ni mgao wa kila siku interval ya siku 2-4 na mara nyingine wiki na hata hayo yanayopatikana kidogo ya mgao yanatiririka kama matone ya damu,tulishasahau kuogea maji ya bombani kwenye nyumba zetu , ni mwendo wa ndoo za kukinga na kununua kutoka kwenye visima.

Sasa bosi wa wizara kashtukia mchezo, report za mwezi excellent 100% lakini output ya upatikanaji wa maji ni only 10% to 20% kachukua report hizo na ujazo,kawaita viongozi Dawasa, kaenda Ruvu, kaenda kwenye matanki makubwa ya kuhifadhia maji Dar, alichokikuta ni ilikuwa surprise kubwa,very contrary na report alizonazo, halafu kibaya Bosi wa Dawasco huyo kaingia mitini wakati wa visit;shame upon his face. Jamaa hana majibu. Kapigwa mkwara na kupewa ultmultum la sivyo ajitathmini kama anafit kwa nafasi hiyo.

Kilichonishtua sasa ni jana,siku ya pili baada ya mkwara, maji yakaanza kutiririka at least yasiyo ya matone, usiku wa leo nasikia mabomba ndani yanatema; mabafuni na vyooni . Kwa kweli kila mtu akashtuka na kushangaa ni kama tumeona kakakuona, ni hadimu sana,mara ya mwisho kuona one of the wonders za dunia kama hizi ni wakati wa mwendazake ndipo tulipata maji hivi.

Swali la kujiuliza mimi na wewe ni, hii inakuwaje? mpaka viongozi wa taasisi nyeti wapigwe mkwara wa kuua mtu ndipo watekeleze wajibu wao,basi kama ndio hivyo viongozi wakuu wizarani na mikoani twende na mwendo huohuo mikoa yote na taasisi zote. Inaonekana kero zetu ni za kusababisha, ni kutokana na uzembe wa mabosi na watumishi wa taasisi husika. Napenda kuwakilisha

Pia soma:

√ - News Alert: - Waziri Aweso amtimua kazi Meneja wa RUWASA wilaya ya Misungwi Marwa Kisibo, kutokana na kushindwa kusimamia miradi ya maji ipasavyo
 
Wengi ni wanufaika wa hiyo Hali ya kushika vyeo halafu kazi hufanyi kesho tu Aweso atakuwa labled katili maana ndiyo namna yetu ya kufanya kazi mabadiliko viongozi hawayataki.
 
Hakuna lolote pale kwa juma uwezo waziri nimeona kabisa ni maigizo kuna vidogo vina online zo tv vimekula posho kututengenezea maigizo.

Wanajua shida ya maji ukiileta sana inaweza kumuondoa huyo waziri
 
Suala la maji Dar ni moja ya ushahidi kuwa nchi yetu itakufa masikini.
 
Wengi tulikuwa tunashangaa nini kimeikumba DAWASA

Kweli wanasikitisha

Kama ni hivi tunalo tatizo kubwa kama nchi.
 
kwani waliopewa kazi ya kutoa huduma kazi zao ni nini?.kuna maisha afrika na wenzetu ukienda kwao utaona kwa nini idara zao zipo kwa ajiri ya nini sio siasa na ujinga kama hapa
kaka yake shetani upo hapa,acha malalamiko shauri cha kufanya.
 
kaka yake shetani upo hapa,acha malalamiko shauri cha kufanya.
MAGU aliujua huu ujinga siku nyingi ndiyo maana aliendesha nchi Kwa mtindo ule na alifanikiwa sana kwenye huduma,Leo umeme umezidi mahitaji lakini unazima mara Tano Kwa siku hapo linatakiwa jicho.
 
Hii nchi wengi wanalipwa mishahara wasiyoifanyia kazi.

Anahitajika kiongozi wa kuwasukuma tu huko maofisini, wakiachwa kidogo wanalala kabisa.

Maji ya Dawasa yalikuwa yanatoka tope kabisa, karibia siku tano, leo ndio afadhali ile rangi halisi ya maji ya bomba imeanza kuonekana.
 
UWAJIBIKAJI ni tatizo kubwa kwetu, kuna sumu imeingia damuni kwa watanzania mtu akiwa kitengo lazima kupiga, RUSHWA kwake ni haki yake, kuna majivuno sana, lazima afanye fyongo hata sehemu isiyo na ulazima atafanya tu.

Sumu mbaya sana hii.
 
Back
Top Bottom