Aliyoandika Boniface Jacob kuhusu mgomo wa wafanyabiara Kariakoo

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Imeandikwa na Boniface Jacob

1. Kabla ya mgomo Wafanyabiashara wamekaa vikao zaidi ya 10 na mamlaka ya mapato TRA, hawakupata majibu.

2. Kabla ya mgomo Wafanyabiashara wamekaa vikao na serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Ilala wakiomba Waziri wa fedha afike kuwa sikiliza lakini Waziri wa fedha hakuwahi kwenda.

3. Mkuu wa Wilaya ya Ilala amepambana sana kuhakikisha mgomo hautokei (Wafanyabiashara wanampongeza) Mkuu wa wilaya ya ilala akaomba Wafanyabiashara wasubiri mwezi mmoja, ili awasiliane na Viongozi wake kwanza

Mwezi ukaisha Mkuu wa Wilaya akapuuzwa na viongozi wake wa Juu.

4. Mkuu wa Mkoa mara zote hizi hakuwahi kuonekana katika vikao chochote cha Wafanyabiashara, wala hakuwahi kusaidia kupeleka malalamiko ngazi za Juu.

Ameonekana Jana tu, ktk Vitisho.

5. Viongozi wa Wafanyabiashara wakaomba waende Dodoma kuonana na Waziri wa fedha ili madai yao yaingizwe katika Bajeti hii na sheria mpya ya fedha- Wakapuuzwa

6. Viongozi wa Wafanyabiashara kupitia kamati yao Maalumu iliyoundwa wakati Waziri Mkuu alipofika Kariakoo iliwajulisha wafanya biashaara wenzao kuwa hoja zao zote 27 zimetupiliwa mbali.

7. Katika hoja zao 27 za awali,Wafanyabiashara wanahoja za haraka 7 zikifamyiwa kazi watafungua Maduka yao wakati watasubiri serikali wafanyie kazi hizo 20.

8. Hoja hizo ni

1. Kupunguza faini ya kuto toa risiti ambayo kwa saasa 15M
2. Kuondoa service levy.
3. Kamtakamata ya TRA mitaani
4. Kunyan'ganywa kwa VAT baadhi ya wafanya biashara
5. VAT kukusanywa bandarini,airport na ktk Mipaka
6. Kuzia wachina na Wageni ktk biashara ndogondogo kariakoo
7. VAT ianze Tsh millioni 500 hadi Tsh billioni 1 ,badala ya sasa ya Tsh million 200

9. Leo saa 7: 00 mchana, Dodoma, Waziri wa fedha na Waziri wa viwanda na biashara watakutana na viongozi wa wafanyabiashara

Msimamo wa wafanyabishara ni kwamba hawataki kusikia lolote kutoka kwa Mawaziri hao baada ya kuongopewa kwa muda mrefu

10. WANATAKA RAIS AENDE KARIAKOO au KAULI YA RAIS KUHUSU HOJA ZAO.
 
Sheria ya VAT ili usajiliwe imeshatoka mauzo ya 100mil mpk 200m?
 
Milion 15 fines .je kama mtaji wako ni milion 2 na Huna hiyo fine
 
2,5 na 7 haviwezi kutekelezeka kabisa. Wala tusidanganyane
 
Hoja ni moja, namba 4.
Zilizobakia utopolo, serikali ikaze buti mgomo uendelee tuone mwisho wa sinema.
 
Hivi Mbunge wa Ilala ameshawahi wasilisha bungeni kero za wananchi wake? ( Wafanyabiashara wa Kariakoo)
 
Imeandikwa na Boniface Jacob

1. Kabla ya mgomo Wafanyabiashara wamekaa vikao zaidi ya 10 na mamlaka ya mapato TRA, hawakupata majibu.

2. Kabla ya mgomo Wafanyabiashara wamekaa vikao na serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Ilala wakiomba Waziri wa fedha afike kuwa sikiliza lakini Waziri wa fedha hakuwahi kwenda.

3. Mkuu wa Wilaya ya Ilala amepambana sana kuhakikisha mgomo hautokei (Wafanyabiashara wanampongeza) Mkuu wa wilaya ya ilala akaomba Wafanyabiashara wasubiri mwezi mmoja, ili awasiliane na Viongozi wake kwanza

Mwezi ukaisha Mkuu wa Wilaya akapuuzwa na viongozi wake wa Juu.

4. Mkuu wa Mkoa mara zote hizi hakuwahi kuonekana katika vikao chochote cha Wafanyabiashara, wala hakuwahi kusaidia kupeleka malalamiko ngazi za Juu.

Ameonekana Jana tu, ktk Vitisho.

5. Viongozi wa Wafanyabiashara wakaomba waende Dodoma kuonana na Waziri wa fedha ili madai yao yaingizwe katika Bajeti hii na sheria mpya ya fedha- Wakapuuzwa

6. Viongozi wa Wafanyabiashara kupitia kamati yao Maalumu iliyoundwa wakati Waziri Mkuu alipofika Kariakoo iliwajulisha wafanya biashaara wenzao kuwa hoja zao zote 27 zimetupiliwa mbali.

7. Katika hoja zao 27 za awali,Wafanyabiashara wanahoja za haraka 7 zikifamyiwa kazi watafungua Maduka yao wakati watasubiri serikali wafanyie kazi hizo 20.

8. Hoja hizo ni

1. Kupunguza faini ya kuto toa risiti ambayo kwa saasa 15M
2. Kuondoa service levy.
3. Kamtakamata ya TRA mitaani
4. Kunyan'ganywa kwa VAT baadhi ya wafanya biashara
5. VAT kukusanywa bandarini,airport na ktk Mipaka
6. Kuzia wachina na Wageni ktk biashara ndogondogo kariakoo
7. VAT ianze Tsh millioni 500 hadi Tsh billioni 1 ,badala ya sasa ya Tsh million 200

9. Leo saa 7: 00 mchana, Dodoma, Waziri Kila hatua wa fedha na Waziri wa viwanda na biashara watakutana na viongozi wa wafanyabiashara

Msimamo wa wafanyabishara ni kwamba hawataki kusikia lolote kutoka kwa Mawaziri hao baada ya kuongopewa kwa muda mrefu

10. WANATAKA RAIS AENDE KARIAKOO au KAULI YA RAIS KUHUSU HOJA ZAO.
Wataalamu wa Kodi watusaidie uelewa
Nchi tunalipa Kodi ya vat Kila hatua ya ununuzi,
Cha msingi wasikizwe hoja zao zijibiwe kitaaalamu kwenye mdahalo wa wazi ambao utakuwa televiside

Tukubali uzalendo umepungua watu hawana Ari ya kulipa kodi Wakiona ripoti za CAG zinazoripoti ubadjirifu mkubwa
 
Hoja ni moja, namba 4.
Zilizobakia utopolo, serikali ikaze buti mgomo uendelee tuone mwisho wa sinema.

Kwa sababu huna uelewa.

Kanuni ya kodi duniani kote, huwezi kumtoza mtu kodi ile ile kwa zaidi ya mara moja kwa bidhaa ile ile.

Kama VAT inatozwa wakati wa importation, basi ibakie huko tu, na siyo tena kwenye mauzo. Kama wanatakata itozwe kwenye mauzo, basi waiondoe wakati wa importation. Ujinga wa kutoza kodi zaidi ya mara moja kwa bifhaa ile ile ndiko kunakofanya bidhaa hapa Tanzania ziwe aghali kuliko mataifa ambayo yanapitisha bandari ya Tanzania. Yaani unashangaa wafanyabiashara wanaenda kununua bidhaa Uganda zilizopitia Dar Port, kwa sababu zina bei nafuu kuliko akinunua Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom