Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Heshima zenu wakuu. Hongereni kwa kazi. Na mnaopumzika, hongereni kwa mapumziko.
Haya, twende kwenye mada.
Mambo mengi yanayotokea nyakati hizi duniani, yalitabiriwa na manabii wa Mungu miaka mingi iliyopita, na kuandikwa katika Biblia. Yesu Kristo pia alipokuwa duniani, alinena mambo yatakayotokea duniani na akasema kwamba tutakapoyaona au kuyasikia basi tujue kuwa hiyo ni ishara au dalili ya kurudi kwake, na ya mwisho wa dunia. Jambo mojawapo alilolitaja limeandikwa katika Mt 24:6. “Nanyi mtasikia habari za vita na tetesi za vita.”
Rais Trump (katika kikao kizito na Rais Zelensky) ameonekana na kusikika kote duniani akimwambia Rais Zelensky kuwa anacheza na Vita Kuu ya III(gambling with World War Three). Tetesi ya Vita Kuu ya Tatu hiyo imetamkwa na Rais anayeongoza Taifa lenye silaha na teknolojia za kisasa, zinazoweza kusababisha Vita Kuu ya Tatu.
Ndugu zangu, dalili za kuja kwa Yesu hizo zinaendelea kutimia. Hivyo tuendelee kujiweka tayari kumlaki Yesu Kristo kwa kuishi maisha matakatifu. Tusisahau Yesu atakuja ghafla, katika siku na saa wasiyoitarajia wengi(Mathayo 24:44).
Asiyejali maneno haya aendelee kutenda mabaya, “atakiona cha mtema kuni.” Aliye mchafu na aendelee kuwa mchafu, “atakiona kilichomnyoa khanga manyoya.” Atendaye haki na aendelee kutenda haki, na yeye aliye mtakatifu na aendelee kuwa mtakatifu maana atapata thawabu. Ufunuo 22:10-12.
Hold fast to wisdom, for the days foretold are unfolding before our eyes.