Allan Quatermain

Allan Quatermain

Musia

Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
95
Reaction score
19
Wapendwa natafuta kitabu cha hadithi kinachoitwa 'Mambo ya Ajabu Yaliyompata Allan Quatermain na Wenzake' tafsiri ya Kiswahili. Je, kuna sehemu yoyote ndani ya Tanzania nitakipata hiki kitabu?
 
du zamani tulikuwa stori hizo tulikuwa tunazikariri vichwani, nangoja kusikia vinakopatikana
 
Umenikumbusha Umsolopogas "Mwana wa Mfalme Chaka", Sir Henry Curtis, Nyleptha, Solais kwenye nchi ya Wazuvendi
 
Wapendwa natafuta kitabu cha hadithi kinachoitwa 'Mambo ya Ajabu Yaliyompata Allan Quatermain na Wenzake' tafsiri ya Kiswahili. Je, kuna sehemu yoyote ndani ya Tanzania nitakipata hiki kitabu?

Kiliandikwa na Henry Rider Hagard, mwingereza aliyepata kuishi Natal wakati fulani.
Nilipata kuwa na nakala moja chakavu sana, panya waliitoboa na kurasa kadha wa kadha zimenyofoka. Sidhani kama ingekufaa...
 
Hahahaaa, nimekumbushwa mbali. Na ile shoka iliitwaje?Inkosikazi au?
 
Je, naweza kupata wapi kile cha 'Mlima kolelo' na 'Mashimo ya Mfalme Suleiman'?
 
...Kinaitwa ' Hadithi ya/za Allan Quarterman'. Jaribu pale duka la Vitabu mtaa wa Samora karibu na Extelcomms. Unaweza kukipata japokuwa kitakuwa toleo la kisasa na sio lile tulilosoma sisi mwaka 47
 
hahahaaa, nimekumbushwa mbali. Na ile shoka iliitwaje?inkosikazi au?

hujakosea maana yake mke wa mfalmenakunbuka lilipasuka vipandevipande baada ya kuuvunja mwamba mtakatifu
 
je, naweza kupata wapi kile cha 'mlima kolelo' na 'mashimo ya mfalme suleiman'?

nakumbuka maeneo ya kisutu sokoni kuna jamaa wanauza vitabu vya zamani mimi nilivipata hapo "machimbo ya mfalme suleman na alfu lela ulela
 
Nilisoma story ya umsolopagas,kumbe was a true man,tafuta around samora Ave, unaweza ukapata mkuu!
 
Nenda katika duka la TPH mitaa ya Posta. Nilivikuta nkanunua hadi nkaviacha.
 
pia sio mbaya ukitafuta movie hii

'THE LEAGUE OF EXTRA ORDINARY MEN'

NI MOVIE ILIYOTENGENEZWA NA HISTORIA YA ALAN
 
Je, naweza kupata wapi kile cha 'Mlima kolelo' na 'Mashimo ya Mfalme Suleiman'?

hiyo mlima kolelo niliiona muvi yake mda kidogo ukikosa kitabu tafuta muv

dah huyo Allan na yenyewe nimeiangalia long sana kwe kumbi za video so mkikosa vtabu tafuten hata muvie zake kwenye maliblary.
 
hiyo mlima kolelo niliiona muvi yake mda kidogo ukikosa kitabu tafuta muv

dah huyo Allan na yenyewe nimeiangalia long sana kwe kumbi za video so mkikosa vtabu tafuten hata muvie zake kwenye maliblary.
Mkuu ushauri mzuri huu, unaweza kutuongoza mahali ambapo tunaweza kuzipata.
 
Back
Top Bottom