loykeys
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 1,175
- 910
Wasalaam wana jamvi JF Doctor,
Jamani naombeni msaada wenu kuna kipindi cha mwaka 2007 nilianza ghafla kupata uvimbe kama majipu hivi usoni na kwenye nyama za sikio (sehemu wanayovaa hereni dada zetu) yaani nilikuwa navimba mpaka sura ikawa imeharibika kwa kuwa na makovu ya vidonda na kipindi hicho nilikuwa nasoma advance shule moja mixture huko bagamoyo, da ikabidi niwe najifungia dormitory mpaka uso upoe ndo natoka nje. Uongozi wa hiyo shule wakachukua hatua ya kunipa ruhusa nikafanyiwe vipimo. Kweli nikafanya vipimo vya allergy katika clinic moja ipo mjini, yaan sikuamini masikio yangu kuna vitu niliambiwa ndo vinanisababishia nipate kuchafuka uso na kuvimba na wakati mwingine macho kuvimba na kuwasha pamoja na kupata flu kali.
Vipimo vilionyesha nina allergy ya vyakula aina ya 'white meat' yaani samaki, nyama ya kuku, bata, jamii yote ya dagaa, mayai hiyo ni kwa upande wa misosi, allergy nyingine ni house dust, pollen, vitu vyenye harufu kali kama perfume, petrol au kerosene, manyoya ya paka, ng'ombe na kuepuka kuingia kwenye mabanda ya kuku au kuvuta hewa ya huko mabandani. Niliwauliza kuhusu kama kuna uwezekano wa kupata matibabu walinambia kinga pekee ni kutotumia hivyo vyakula pamoja na hivo vitu walivonikataza. Na kweli nilivofuata ushauri wao niliona mabadiliko lakini kila nilipojaribu kutumia kimoja wapo kati vyakula nilivyodhuiwa hali ile kuvimba ilijirudia baada ya masaa 48.
Kwa kweli sasa ni miaka saba imepita na nimekuwa nikiishi katika hiyo hali bila kula kuku, samaki, dagaa, mayai nimekuwa mtumwa wa red meat na imefikia kipindi nimechoka kula nyama nyekundu nataka nianze kula white meat, msaada please mwenye kujua kama kuna matibabu ya allergy hii kwa kweli anisaidie nahitaji matibabu......:angry:
Asanteni...!!