Allergies are killing me... Msaada please!

loykeys

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Posts
1,175
Reaction score
910
Wasalaam wana jamvi JF Doctor,
Jamani naombeni msaada wenu kuna kipindi cha mwaka 2007 nilianza ghafla kupata uvimbe kama majipu hivi usoni na kwenye nyama za sikio (sehemu wanayovaa hereni dada zetu) yaani nilikuwa navimba mpaka sura ikawa imeharibika kwa kuwa na makovu ya vidonda na kipindi hicho nilikuwa nasoma advance shule moja mixture huko bagamoyo, da ikabidi niwe najifungia dormitory mpaka uso upoe ndo natoka nje. Uongozi wa hiyo shule wakachukua hatua ya kunipa ruhusa nikafanyiwe vipimo. Kweli nikafanya vipimo vya allergy katika clinic moja ipo mjini, yaan sikuamini masikio yangu kuna vitu niliambiwa ndo vinanisababishia nipate kuchafuka uso na kuvimba na wakati mwingine macho kuvimba na kuwasha pamoja na kupata flu kali.

Vipimo vilionyesha nina allergy ya vyakula aina ya 'white meat' yaani samaki, nyama ya kuku, bata, jamii yote ya dagaa, mayai hiyo ni kwa upande wa misosi, allergy nyingine ni house dust, pollen, vitu vyenye harufu kali kama perfume, petrol au kerosene, manyoya ya paka, ng'ombe na kuepuka kuingia kwenye mabanda ya kuku au kuvuta hewa ya huko mabandani. Niliwauliza kuhusu kama kuna uwezekano wa kupata matibabu walinambia kinga pekee ni kutotumia hivyo vyakula pamoja na hivo vitu walivonikataza. Na kweli nilivofuata ushauri wao niliona mabadiliko lakini kila nilipojaribu kutumia kimoja wapo kati vyakula nilivyodhuiwa hali ile kuvimba ilijirudia baada ya masaa 48.

Kwa kweli sasa ni miaka saba imepita na nimekuwa nikiishi katika hiyo hali bila kula kuku, samaki, dagaa, mayai nimekuwa mtumwa wa red meat na imefikia kipindi nimechoka kula nyama nyekundu nataka nianze kula white meat, msaada please mwenye kujua kama kuna matibabu ya allergy hii kwa kweli anisaidie nahitaji matibabu......:angry:

Asanteni...!!
 
Pole sana! Kwakweli si rahisi kuondoa allergy ... jaribu ku alternate na mboga mbalimbali za majani kuna variety nyingi nzuri sana za mboga za majani please explore that and am sure you will enjoy . Just forget about white meat isn't worthy it. pia punguza red meet si nzuri kwa afya ...
 
Kwanza pole sana.
Pili nitoe ushauri wangu; Allergy ama kama nisikiavyo waswahili wakiita MZIO/ MIZIO haitibiki kwa dawa ILA HUTULIZWA TU.

Ipo njia mojawapo ambayo hutumika katika nchi zilizoendelea kimatibabu ambapo mgonjwa hudungwa/ huchomwa sindano za allergens kwa muda fulani ili mwili ujizoeze ILA HAIJAZAA MATUNDA, njia maarufu inayosaidia ni ile ya kudunga sindano ya antihistamines kila baada ya kipindi fulani pamoja na kunywa vidonge.

Njia ya kwanza kabisa ambayo unaweza kusaidika ni kwa kutambua allergens zinazokuathiri ni zipi kupitia njia ya kupima kama ulivyokwishafanya HALAFU KUCHUKUA HATUA YA KUJITENGA NAVYO KABISA.
Kuna baadhi ya reactions zinaweza kutibika baada ya kipindi fulani cha kujitenga na allergens husika. Yaweza kuwa miaka 10 ama zaidi. Kumbuka hili halitokei kwa kutibiwa bali mwili kujirekebisha wenyewe (histamines balance).
Kimsingi allergy reaction hutokea kutokana na body chemical(s) imbalance (esp. Histamines).

Njia ya pili ni kupata huduma ya maombi kwa jina la Yesu Kristo. Japo hili nimelitaja kama la pili ila ni la kwanza na linahitajika kwa hatua yoyote KUMUOMBA MUNGU.
Kwanini kumuomba Mungu? Yeye ndiye Muumba wa vyote na ana uwezo juu ya vitu vyote, yeye huwapa matabibu maarifa kutibu wagonjwa naye mwenyewe Mungu muumba ndiye huwaponya wagonjwa hao.

PIA NI KWELI ALLERGY INAUA KWA URAHISI SANA.
 
Shukrani mkuu na thanks kwa kunifariji najiandaa katika maisha mapya ya kuwa vegetarian. Mwanzo mgumu lakini sina jinsi nitakubaliana na khali hii nitazoea.
 

Asante sana mkuu umenifafanulia vizuri na umeielezea kitaalamu zaidi, ww ni specialist wa haya mambo? naomba nichukue ushauri wako pengine utanisaidia na pia hiyo option ya pili ambayo ingekuwa ya kwanza pia ni njia nzuri kwa imani tuu inawezekana.... walimwengu wa leo wanasema "marufuku kukata tamaa" Asante sana
 
kapime kuna allergy test ili ujue una allergy ya nini badala ya kubahatisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…