X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,400
- 14,339
Alli Migeyo maarufu kama "ALLI MATATA" ni Mtanzania wa kwanza kupigwa bomu la machozi. Alipigwa mabomu manne ya machozi Desember 2, 1953.
Alipigwa mabomu hayo na askari wa kikoloni wa kiingereza wakati akiendesha kikao cha TAA (Tanganyika African Association).
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na kitabu cha " MWITO WA UHURU" cha mwaka 1961 yanaeleza Desember 6, 1953 chama kiliitisha mkutano wa dharula kwa ajili ya manung'uniko na kupeleka malalamiko kwa utawala wa kikoloni na kutaka iwe mwanzo na mwisho kutumia mabomu ya gesi katika ardhi ya Tanganyika.
ALLI MIGEYO alipewa jina la ALLI MATATA na mzungu aliyeng'atwa kidole na ALLI chanzo chake kikiwa ni kupinga sheria kandamizi za kikoloni.