Napenda kuchangia kidogo mada yako mimi ni mdau wa mambo haya. Nadhani kwanza tuweke sawa baadhi ya mambo, UFO inasimamia au ni kifupi cha Unidentified Flying Object kwamba kifaa fulani kimeonekana angani lakini hakijulikani ni kitu gani. UFO sio viumbe kwa hakika bali vitu vinavyoweza kuwa na viumbe ndani yake kutokana na concept ya zamani kwamba kila kinachoruka kinaeza kuwa na rubani hilo moja lakini pia hata kama hakina rubani kama kinaruka na sio ndege au vifaa vingine tunavyovitambua basi vyaweza kuwa vimetoka nje ya anga letu na labda ndani yake kuna viumbe kutoka anga nyingine.
Uwepo wa viumbe wengine nje ya Dunia
Ni ukweli kwamba kuna nyota nyingi sana, na baadhi zinafanana na Jua letu na pia zina sayari zinazozizunguka tena baadhi ya sayari zina mazingira kama ya Dunia. Kwa probability sayari zinazofanana na Jua (our host star) ni mabilioni, hii inafanya pia uwezekano wa kuwepo Earth-like planet au sayari zifananazo na Dunia kuwa mkubwa.
Katika galaxy tuliyomo pekee ya Milky Way kuna zaidi ya nyota billioni mia moja (100) na ulimwengu unaoweza kuonekana (inawezekana ulimwengu hauna kikomo) una galaxies zaidi ya bilioni mia moja. Katika miaka ya karibuni tumegundua kwamba katika baadhi ya nyota hizi nyingi sana, zipo zinazofanana na Jua letu au nyota inayo-support uwepo wa Dunia na uhai (through gravitational pull na solar activity).
Kitu kingine ni kwamba nyota nyingi zina sayari zinazozizunguka (planetary systems), baadhi ya sayari hizi zina mazingira kama ya dunia. Hakika ilikuwa vigumu kidogo kujua kama kuna sayari nyingine nje ya mfumo wa jua, maana sayari hazitoi mwanga kama zilivyo nyota na kwa teknolojia ya zamani mwanga (luminosity) ulikuwa kigezo kikubwa cha kuona vitu hivi vilivyo mbali sana. Lakini sasa tunajua kwa hakika juu ya kuwepo sayari nyingi katika mifumo mingi ya nyota.
Vivyo basi kutokana na namba kubwa sana ya nyota ambazo pia zinahusishwa na kuwepo kwa sayari pengine kwa idadi sawa au zaidi ya nyota basi pia probability ya kuwepo uhai sehemu nyingine katika Universe ni kubwa maradufu.
Lakini jambo moja ni kuwa unapotafuta uhai au viumbe wengine kwa matarajio ya kuona watu, ngombe au wadudu hili linaweza lisiwepo hata kwa kudhani tu kwamba watafanana kidogo au watakuwa at least na pua na macho. Utapotea. Kila kitu kilichopo katika Dunia kiko kama kilivyo kwa kuwa mazingira haya tuliyomo ni sababu kubwa ya viumbe kuwa kama vilivyo. (mtazamo wa evolution). Hivyo basi viumbe au uhai wa aina tofauti katika sehemu tofauti ya Universe kutokana na tofauti za mazingira uhai huu utachukua mikondo tofauti na mbali kabisa na a jinsi mkondo huu wa uhai katika Dunia ulivyochukua.
Kwa kuwa uhai huu ume-evolve kwa muda fulani basi kama ikitokea kuna uhai wa aina fulani sehemu nyingine ya universe kwa muda mrefu zaidi sana kulinganisha na huu wa Dunia basi ni wazi viumbe hao watakuwa pia wako mbali zaidi yetu katika intelligence. Hawa ndio tunawaita other intelligent beings in the universe. Kama hawa intelligents beings wako katika eneo moja nasi hatujawaona au hawajatuona hii inawezekana kabisa kutokana na sababu nyingi ambazo sitazielezea kwa sasa. Kama wametuona na wamekaa kimya au wanatuchunguza pia hili linawezekana na nina sababu za msingi juu ya hili.
Suala moja la msingi katika swali lako ni kwamba je tuko salama (sisi kama viumbe wa duniani wenye uelewa) kama kuna viumbe wengine wenye uelewa mkubwa maradufu kuliko sisi?, na jibu kwa logic ya kawaida ni kwamba hatuko salama.
Kwa sisi waafrika tunaweza kuufananisha ujio wa viumbe wenye nguvu kubwa, uelewa na maendeleo makubwa kama wakoloni kutoka Europe walivyoingia Africa. Na si Africa pekee, katika historia na kumbukumbu za simulizi zote haijawahi kuwa ahueni kwa wenyeji pale jamii yenye nguvu inapogundua eneo jipya lenye jamii siyo na nguvu. Wahindi wekundu wa America, Aboriginals, Africans, Wahindu, na jamii nyingine za Dunia zimeshuhudia ubaya wa wageni wenye nguvu zaidi wanapoingia katika eneo la wenyeji wanyonge.
Pia katika Europe ya zamani kuna historia zaidi yenye kuonyesha mabavu makubwa ambapo huenda hulka ya ukoloni ilijengwa huku. Kuna wale Vikings katika Ulaya ambao kwa ustadi wao wa vita jamii nyingi ziliumia pale walipozunguka pwani mbalimbali kuvuna wasichopanda.
Pengine sisi ni viumbe dhaifu ambao tunaweza geuzwa watumwa au jinsi yoyote ya viumbe wenye nguvu kujipatia faida ya uwepo wetu. Pengine sisi ni tishio kwao kwa jinsi tunavyozidi kuelewa mambo na kuongezeka. Pengine sisi tunakosea pale tunapotuma signals katika outer space bila kujua tunamwita adui. Ni ukweli kwamba SETI wamekuwa wakituma signals ili intelligent being yeyote aliye huko katika anga za mbali anaweza sikia na akatujibu. Hatari kubwa hii kama vile ndama aliyeko peke yake msituni anavyojaribu kuwatafuta wenzie kwa mlio bila kujua simba na chui nao wako eneo hilo.
Natumai umepata mwanga kidogo.
Kwa mfano huu asiyeelewa hastahili kuitwa binadamu. hapa ni sawa na kupeleka umeme kijijini. .. .. .. . Heshima kwako Monstgala.
UFO sio Alliens ....
Halafu kwanini hawaji huku Africa?
Mie nauliza tu iwapo naweza kumuoa mmojawapo
umeniwahi....hata Bara Asia hawaendi na wakienda ni China tu na pia Australia. Au wananusa umaskini na wanaukimbia?
Mkuu Utingo hili ni swali safi nami nilitaka kuuliza au wazungu na wenzao wanachezea tu akili zetu na mateknologia yao...???
UFO sio Alliens ....
Halafu kwanini hawaji huku Africa?
Mbona mitume na manabii wote wanatokea huko kwao i.e ni weupe hilo hamhoji-mnahoji hili lisilo na madhara makubwa,...miafrika bhana.
Mungu yupi huyu?ahahahahahaaaaaaaaaaaa,...ni sawa na vile Mungu alivyoisahau Afrika mpaka akawatuma wazungu na waarabu kutuletea ujumbe wake...tafakari - then chukua hatua mkuu.
alien and UFOs ni strategies ambazo zimetengenezwa kitambo ili kufanikisha issue ya NWO.....
Hakuna :alien: hata mmoja hapa duniani.... na hizo UFOs znazo onekana youtube watu wame upload ni kweli zinaonekana ni UFO lakini ukweli they are man - made (Hologram technology) ....
hivyo kuna mambo ya project blue beam, CERN na issue yake ya LHC ambazo zote zita link issue ya alien threats as far as I know...