Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Baada ya mh Rais Samia kupiga indiketa ya kuutumbua uongozi wa mkoa wa Mara, leo Ally Hapi katumia jukwaa vizuri kujitetea.
Pamoja na ukweli kuwa Ally Hapi angeweza kuyatatua yote aliyomwomba Rais , lakini wachunguzi wa mambo wanafikiri Ally Hapi bado hajawiva kiuongozi.
Wakurugenzi ndani ya mkoa ndani ya wilaya wanaomsaidia DED bado wako ndani ya mamlaka ya kusimamiwa na kuchukuliwa hatua na Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa kushindwa kuwasimamia watendaji na hata wateule wa Rais mkoani kwake ni kushindwa kazi.