Nchi inaliwa mno. Siyo mkoa wa Mara pekee, bali nchi nzima inaliwa kipuuzi sana na wajanja. Kuanzia kwenye majiji, miji, na hata vijijini huko, upigaji umeshika kasi. Pesa zinaingia na kupigwa kimya kimya huku shughuli za maendeleo zikiachwa bila kufanyika.
Kwakweli mama anatakiwa ajipange sana kupambana na hawa wezi na wapigaji. Mifumo ya nchi inampa Rais wigo mpana wa kufanya chochote atakacho. Asipoyatumia mamlaka hayo, lawama zote ni kwake.
Mama asipoangalia atajikuta anaondolewa madarakani hata kwa maandamano. Sisi wanyonge ndiyo tunapita barabara za mashimo, tunakosa huduma za maji, tunanunua mahitaji bei ghali, na kuumizwa kwa njia nyingine nyingi kila siku.