Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ndugu Ally Hapi, ametoa onyo kali kwa viongozi wa Serikali za vijiji wanaotokana na CCM, akiwataka kuacha tabia ya kujiona miungu watu kwa kuwaonea wananchi na kupora mali zao.
Akizungumza katika mkutano wake na wanachama wa chama hicho katika Halmashauri ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Hapi alisema kuwa chama hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi wanaokwenda kinyume na misingi ya uadilifu na haki.