Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ally Hapi, amesema kuwa CCM ndicho chama pekee chenye uwezo wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi, huku akidai kuwa vyama vingine vina nia ya kutafuta madaraka pekee.
Hapi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanachama wa CCM wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma, alipowasili kwa ziara ya siku moja yenye lengo la kukijenga chama na jumui