Ally Kleist Sykes na Kenneth David Kaunda, 1953

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Utangulizi
Barua hiyo hapo chini kutoka Ikulu inasema kuwa uhusiano wa Zambia na Tanzania ulianzishwa na Baba wa Taifa.

BARUA%2BKUTOKA%2BIKULU.jpg

Ningependa kwa faida ya historia ya taifa letu lau kwa mukthasari ninyanyambue yale niliyokutananayo katika Nyaraka za Sykes wakati natafiti maisha ya Abdul Sykes ili niweke wazi chanzo cha uhusiano wa Tanganyika (Tanzania) na Northern Rhodesia (Zambia) wakati wa harakati za Afrika kudai uhuru wake katika miaka ya 1950.

Uhusino wa Tanzania na Zambia rekodi za kihistoria zinaonyesha ulianza mwaka wa 1953 wakati Ally Sykes alipoanza kuandikiana barua na Kenneth Kaunda akiwa kiongozi wa Pan African National Congress.

Hayo hapo chini ni kutoka katika kitabu cha Maisha ya Abdul Sykes:

Kulia: Abdul na Ally Sykes 1942 wakiwa katika King's African Rifles Vita Kuu ya
Pili ya Dunia (1938 - 1945) Burrma Infantry

‘’Abdulwahid alipoanza shughuli zake za siasa na Chama cha Makuli, Ally alianza siasa kama alivyoanza kaka yake na chama cha wafanyakazi - Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA). Madai ya kisiasa katika TAGSA ndiyo yaliompa Ally umaarufu katika TAA na ni mchanganyo wa harakati zote mbili kupitia uongozi wa Ally ndiyo uliyoifanya TAA kujulikana na kutambuliwa nje ya mipaka ya Tanganyika kama chama cha ukombozi. Kutokana na sababu hii wanahistoria wanahitaji vilevile kutafiti kidogo kuhusu Ally Sykes na ni kwa kupitia kwake sehemu ya mapambano ya uhuru wa Tanganyika na maisha ya awali ya Nyerere katika siasa yanaweza kuelezwa. Vilevile ni kwa kupitia kwa Ally Sykes historia inaweza kufahamu namna Nyerere alivyoweza kupanda hadi kwenye madaraka na kuongoza moja ya vyama vya siasa vilivyokuwa na nguvu na mshikamano mzuri sana katika Afrika. Halikadhalika kupitia kwa Ally Sykes mtafiti anakutana na wazalendo wengine wa Tanganyika kama Dennis Pombeah, Dr William Mwanjisi, Dr Michael Lugazia, Rashid Kawawa na wengine wengi. Hivyo hivyo kupitia kwa kaka yake mtu hukutana na watu mashuhuri kama Mwapachu, Nyerere na Kenyatta, kwa kupitia kwa Ally Sykes vilevile mtu anatambulishwa kwa wazalendo wengine wa Afrika kama Tom Mboya na Kenneth Kaunda.

Mwaka wa 1953 Harry Nkumbula alikuwa amechaguliwa rais wa ANC na Kenneth Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini. Mwezi Agosti Kaunda akawa Katibu Mkuu wa ANC. Haukupita muda Kaunda akaanza kupeleka barua Nairobi, Dar es Salaam na Johannesburg akiitikia rai ya Kenya African Union na South African ANC kuwa ëLusaka inapasa kuwa mahali pa kukutana wazalendo kutoka nchi zilizo Kusini mwa Sahara.íUjumbe wa watu watatu wa TAA ulialikwa na Katibu Mkuu wa African Congress ya Northern Rhodesia, Kenneth Kaunda, kuhudhuria mkutano wa Pan African Congress (ANC) mjini Lusaka. Mwezi wa Novemba Ally Sykes alipokea barua kutoka kwa Kaunda akimwalika kuhudhuria mkutano huo. Wakati ule ANC ilikuwa na manungíuniko kadhaa dhidi ya Waingereza na ilikuwa imeamua katika mapambamo yake kutumia njia za amani ambayo katika barua ambayo Kaunda alimpelekea Ally Sykes aliielezea njia hizo za amani kama hivi, ‘’Hutashirikiana na mtu yoyote katika shauri lolote litakalokuwa na madhara kwa maslahi ya Waafrika.’’ (Nyaraka kutoka kwa Kenneth Kaunda kujua kwa Ally Sykes: ANC Circular No. B.1/54 Sykes' Papers).

Hii ilikuwa mwaka wa 1953.

Miezi ya mwisho ya mwaka 1953 uongozi wa TAA makao makuu ulikuwa na shughuli nyingi. Ujumbe wa watu watatu wa TAA ulialikwa na Katibu Mkuu wa African Congress ya Northern Rhodesia, Kenneth Kaunda, kuhudhuria mkutano Pan African Congress (ANC) mjini Lusaka. Mwezi wa Novemba Ally Sykes alipokea barua kutoka kwa Kaunda akimwalika kuhudhuria mkutano huo.

(Angalia Fergus Macpherson, Kenneth Kaunda of Zambia, Lusaka, 1974 uk. 430. Maelezo mengine ya ziada kutoka kwa Ally Sykes).

Kitu ambacho huwasisitizia wana-historia wa hapa nyumbani ni kuwa wasiiogope historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika wawe na ujasiri wa kuitafiti historia hii kabla ya Baba wa Taifa hajapandishwa katika jukwaa la TANU Viwanja Vya Mnazi Mmoja 1954 kuwahutubia wananchi akitanguliwa na Sheikh Suleiman Takadir kama mtambulishaji na muhamasishaji umma.

Kuna mengi wanakosa kwa kuwapuuza hawa wazee wetu.

Baba wa Taifa akiwa na Sheikh Suleiman Takadir Viwanja Vya Mnazi Mmoja. Wengine ni Bi. Titi Mohamed, Rajab Diwani, Clement Mohamed Mtamila, Mama Maria Nyerere...picha hii alinipatia Jim Bailey rafiki yake Ally Sykes aliyekuwa mmiliki wa gazeti la Drum.

Si kweli kuwa uhusiano huu wa Tanganyika (Tanzania) na Zambia aliuanza na Baba wa Taifa. Ulikuwapo hata kabla ya TANU kuundwa 1954.
 
Kwahiyo Ikulu yetu ilikurupuka kama kawaida yao.......
Xavia,
Sidhani kama walikurupuka.

Nadhani tatizo ni kutokuelewa historia ya taifa letu na hii ni kwa
kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika haijaandikwa sawasawa.

Naingia Maktaba nikutafutie historia ya Abdul Sykes na Jomo
Kenyatta
, 1950:

HISTORIA YA JOMO KENYATTA NA ABDULWAHID SYKES 1950
Mohamed Said April 05, 2016 0
Utangulizi

Leo nilipokuwa nikipitia gazeti la Mwananchi (Jumanne Aprili 5, 2016) nilikuta kipande hicho hapo chini kuhusu Jomo Kenyatta:
IMG-20160405-WA0080.jpg

Si wengi wenye kuijua vyema historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika. Hii imesababisha kwa historia hii kubaki kizani takriban sasa inakaribia miaka 70. Mpenzi msomaji nimeona baada ya kusoma na kuona kuwa leo ndiyo siku Jomo Kenyatta alihukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani ni aula nikaiadhimisha siku hii kwa kukunyambulia habari za Jomo Kenyatta kutoka vyanzo vya Tanganyika ya wakati ule.
Hapo chini nakunyambulia histori ya Jomo Kenyatta na Abdulwahid Sykes kama nilivyoandika katika kitabu changu, ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1950)...''

YhA73nxTrRSSxcsKu8BYcrnD_y0y137b_JeukBx724bZ2gAZPa88NwpSJwV20NWzOD7NviuHYNori5gSSfxyhueutiz531IW16JiIfPvDihGEU-xh7qMYqbwGws3sbcYmXAIORwK3fOyIatNJPipbTxQbv-JzCe-zU30-irQfEqZ4Fpttxh7qoY_eT7KhzfGzbYJuzvMIj8DSBJjQMhbAot4J5XMFA2FMgWoZirzR1mdEySxs3VdXR2rWlEJp3vRzUpWAnjyXlIu8WeG6DvB6dbrv-4GTkUKlAv3YnQ27Nf-eS4ASGCv7mYerapZje5Ok6a6UjPdsevYazknB1pH5aZ-nq01BM8m46eCVUttXkX9JBN4Fy2fXtr1x6T8dJN4tyTjXOFdHPshGwSB7weaGE14WOVJOpAvJa38im29-bTNdxQAld_Akgg1FUo9AQA6jhmFrNbMoPD8__w6-a3EhhJ1NBW2Cunx9mj4Uz36LeCvzyF3_x334c8MvcDRvtcq3iL-nvZWTGsKez-7yioJq8BgZ4b1VcTcbSmgQ-1L1ZBGNA3N-nGJ7isxEzuDOrvbWUuc=w940-h690-no

''Mwaka 1950, Abdulwahid alisafiri kwenda Nairobi kukutana na Jomo Kenyatta ili kuanzisha uhusiano na Kenya African Union (KAU).Abdulwahid alifunga safari hii wakati wa mashindano ya kandanda ya Kombe la Gossage. Haya yalikuwa mashindano ya kila mwaka ambayo nchi tatu za Afrika ya Mashariki pamoja na Zanzibar zilikuwa zikishiriki. Huenda Abdulwahid alichagua wakati huu mahsusi ili kuficha dhamiri ya safari yake. Kama mtu labda angetaka kujua sababu ya safari yake ingewezekana kwa urahisi kabisa kuelezwa kuwa alisafiri kwenda Nairobi kutazama mashindano ya Gossage. Abdulwahid alifikia Railway Hotel na alikwenda kuonana na Kenyatta usiku akifuatana na rafiki yake mpenzi kutoka Zanzibar, mmoja wa wacheza mpira katika timu ya Zanzibar. Abdulwahid na rafiki yake walikwenda nje kidogo ya Nairobi kwenye nyumba moja iliyokuwa imegubikwa na giza na kuzungukwa na walinzi wa Mau Mau. Abdulwahid alikuwa anatarajiwa. Kenyatta alipofahamishwa kuwa Abdulwahid amefika na yupo nje, alitoka kumlaki. Kenyatta alikuwa akimfahamu Ally Sykes tangu mwaka 1946. Inawezekana kuwa kazi ya Abdulwahid ilirahisishwa na uhusiano huu wa Kenyatta na mdogo wake. Mzanzibari huyu aliyemsindikiza Abdulwahid alikutana na Kenyatta na wakapeana mikono. Baada ya kutambulishwa Kenyatta, Abdulwahid, Fred Kubai, Bildad Kaggia na Kungu Karumba waliingia kwenye chumba kingine ambako mkutano ulifanyika. Mzanzibari, rafiki yake Abdulwahid alibakia nje na mlinzi.

scan0025.jpg

Timu ya Tanganyika iliyochukua kikombe cha Gossage mwaka wa 1949
Miaka mingi baadaye Mzanzibar yule, rafiki yake Abdulwahid na sasa akiwa ofisa mwandamizi serikalini alikutana na Rais Kenyatta Ikulu ya Nairobi wakati wa sherehe za uhuru wa Kenya mwaka wa 1963. Jambo la kustaajabisha ni kuwa Kenyatta alimkumbuka kuwa alifuatana na Abdulwahid kwenye ule mkutano pale Nairobi mwaka wa 1950. Kenyatta aliyekuwa akizungumza Kiswahili kibovu chenye lafidhi nzito ya Kikikuyu alimkubusha juu ya ule mkutano. Alimwita mpiga picha wake na wakapiga ya pamoja. Picha hii inapamba sebule ya huyu mcheza mpira wa zamani hadi leo. Vilevile Kenyatta alimtunukia tai yenye rangi za taifa la Kenya.

Ajenda kuu ya mkutano huu ilikuwa namna ya kuunganisha harakati za wananchi wa Kenya na Tanganyika dhidi ya Waingereza. Wakati huo Wakikuyu walikuwa tayari wamekwishaanza mapambano ya silaha na majeshi ya Waingereza na hali ya siasa nchini Kenya ilikuwa ya wasiwasi sana. Inawezekana mkutano huu ulifanyika katika mtaa wa Eastleigh, sehemu ambayo mikutano mingi ya Mau Mau katika miaka ya 1950 kabla ya kutangzwa hali ya hatari ilikuwa ikifanyika.

Mwaka wa 1951 Kenyatta kwa mara nyingine aliitisha mkutano mwingine baina ya KAU na TAA mjini Arusha. Katika ujumbe alioutuma kwa TAAw, Kenyatta alisisitiza kuwa uongozi wa chama cha TAA uende mkutanoni na silaha. TAA iliwateua Abdulwahid, Dossa Aziz na Stephen Mhando kuhudhuria mkutano huo. Abdulwahid alikuwa na bastola aliyopewa wakati wa vita na ofisa mmoja mzungu kama zawadi. Ilitokea kuwa siku ya kuzaliwa ya Mzungu yule ilikuwa sawa na yake na kwa sababu yule mzungu akampa bastola yake kwa ukumbusho. Dossa Aziz alikuwa na bunduki iliyokuwa ikipiga risasi tano kwa mfululizo. Hajuijulikani kama Mhando alikuwa na silaha.

Wajumbe wa TAA walisafiri kila mtu peke yake kupoteza lengo. Dossa Aziz alikuwa wa kwanza kuondoka kuelekea Arusha kupitia Dodoma. Siku zile kulikuwa hakuna barabara ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha. Wasafiri waliotaka kwenda Arusha ilibidi wasafiri wapitie Dodoma. Dossa Aziz alifungasha ile bunduki yake ya risasi tano. Mjini Dodoma, Dossa Aziz alipokelewa na Mwalimu Ali Juma Ponda, katibu wa TAA Central Province. Baada ya kuelezwa na Dossa kuhusu ule mkutano wa TAA na KAU uliopangwa kufanyika Arusha, Ponda aliwaarifu Dossa Aziz kuwa kulikuwa na mapigano makali kati ya Mau Mau na vikosi vya Waingereza yaliyosababisha viongozi wa KAU kusakwa na kukamatwa. Ponda alimfahamisha Dossa kuwa ingelikuwa vigumu katika hali kama hiyo kwa Kenyatta na ujumbe wake kuja Arusha. Dossa Aziz aliamua kuvunja safari ya Arusha na kuelekea Mwanza kwa gari la moshi kukagua matawi ya TAA. Mjini Mwanza, Dossa Aziz alipokewa na Dr Joseph Mutahangarwa, makamu wa rais wa TAA katika kanda ya ziwa.

_AVJHc5YAfy13OXyIfHWLP4Xja8JJacOE4qegLQ1r6RReRSDGKaw2ZJI3R-JhuD6vmnvRnxK1zRhMPiHUT-tBf6TCn_BQbMvEEIau8m_J3E9QTQJY4TRTxKJMgn6CeNdUlKNonXFoqXpxfruueT2YR2jSnd0RUc55wG65FVGpyR8qf9SWunMrKQtTrVaUv8x6jcYAxAyKOSxq_MamSoPgCjK-Pt5x5UnCmxxYepZ2Y8DtQqW81jddcw45ocP-h5HSY5FZLzu91jaLpl_SwlrxwYxJSt3LumHmUHd4P3Y-FTalBKrKFNWH0Nt0JCdjyYJzCDh5lHUA7mzFtIRhR8Ilqotkv_8VyD8tUppCxefVLZynOj-YUCLWEG2g4LIU1qK2mJrdLOZ5gwZCJfjqcwYsip3zhtMOKbstgObF4JEMp8XzdKrvb_qf8ALa-QjBc8mb9aL4a9U_627LyBxcZUxqZ1j_8jPH9t1IuGaf309kb0s2Br8NGV8NF5MPCb5vxiopeQrqTA9mqW8gqZqTL_WPIrrQVkquPg9KDms18GVCyynq7RYXiLiotWPvFCGv0Q409_sHQ=w534-h690-no

Kushoto ni Ali Juma Ponda

Dr Mutahangarwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kufuzu udaktari. Baada ya kuelezwa kuhusu ule mkutano wa Arusha, Dr Mutahangarwa alimwonya Dossa kuhusu hatari ya mwenendo aliokuwa akichukua Abdulwahid kama katibu na kaimu rais wa TAA. Dr Mutahangarwa alimweleza Dossa hatari ambazo TAA na uongozi wake ungezikabili pindi serikali ikigundua kwamba TAA ilikuwa ikijaribu kuunganisha mapambano ya TAA na yale ya KAU. Hofu hii aliyoonyesha Dr Mutahangarwa ilikuwa bila wasiwasi wowote hofu ya kweli kabisa kwa sababu KAU ilikuwa inaunga mkono harakati za Mau Mau na Waingereza waliamini kuwa uongozi wa mapambano yale ulikuwa ukitoka KAU na Kenyatta wakiwa na Kaggia walishukiwa kuwa kati ya viongozi hao. Kutoka Mwanza Dossa alipanda meli hadi Bukoba ambako alipokewa na Chifu Rutinwa pamoja na mwanasiasa mkongwe, Ally Migeyo na Suedi Kagasheki na wanachama wengine wa TAA katika tawi la Bukoba.

DCyWcxhOb8pj1xz0_kRONOZCqRPZAV9i1jTfyfqnn9yJ_78wFXiYCJ-sb46jSDNPXz16a3VtdOCgY7bOC1M-ofcf7yIhE0h2EdzuKCA1tUV5K6Rtt7f_y6mNzafJ1vBZMEPaPWHwdLN5vSrGCTufe9NdZqiyCMRmq3nnntxmbnjSFvasi1dhMSV88L0f0VJjIBpbvSKlnKka5VVCBV97E8FPpFjowjOxYipI93OAACAOTc7b_2ZZavmBQRucik3ZvISa_wPRPXXcvILL-AP615cQLpgl0BZcjMmoG9XfVlyb-x3L2-oCBvyCIKHt5FxnE_AzzUXvyWT1ApU2BQAjovD3vDYMnPz4y_0-OKoMncvvIrQD89DS2Dwt0JyXMoVz7Ts86i5SHjzEJHAnJkZTyelcxshe8TfGqelc1r34Ls4lJFvbgfKYSyItLhS2dVRkJ8BIn3mJsaQ03PWLT93h1UBSSBMUx4VaThHDhAQDxdc-HgRqdfYXoUc39OKQ9sxcz04UnI6x8It-sNYAFv19Wt76_e4_J5IzXcWg3VL0czgVnXnkXEOdelZZxVQXULiY8Ioa=w146-h220-no

Ali Migeyo

Aliporudi Dar es Salaam, Dossa alikamatwa katika stesheni ya gari moshi na kupelekwa Central Police. Kituo hiki kilikuwa mkabala la lango kuu la steshini ya treni. Dossa alipelekwa pale na kuhojiwa. Ofisa wa polisi Mzungu alitaka kujua kwa nini Dossa alikuwa akisafiri na bunduki. Baba yake Dossa Aziz Ally aliingilia kati na Dossa akaachiliwa huru bila ya kufunguliwa shtaka lolote.''

0Y3Z1Xlks2AybT6tg_9YeZXgHuzC-6iULnTJuSPnCsmHlcq5-Ecee2V6oEvJFJqdpMyGoPxnp5IfXm37TihPrwigZQN0BX3hQWNKFLKQb9XKNR4S8WBNgM8f5BgkY7BmjaUm131byad1M42hTTfKsCN_ljBm9Av3sNKJlHjMA4O-b7SDo-lo1tE6cz2_TM0-p-MyedkUWxrbN3vCzO9W8PwTiW-oLKvRxBC_5FnSiQu7_3R2g1F5KX0TmWGdPYHShncXF2Q0rtXiBV3dxb-XjNPuVVzAB_a4O6Gnf6S9ver7z0deOg9-QHUb8S_P5WnQSRAWqrySCl80xZWqRtSfxqe3htVp7q3Ka5pSIpgv4duLWmL2lgy01CL2RvMwXAykYaWawJljDwgioQsMvhMH542Xh8V9ug7VMSjZ-xEsQcbkLfRzzN6xo9LSBgfUyA3TjM__il4HdUs3ykKv0l3p62D6d59wu9Dg2UOHWvgnmoM-5hl0C65AuHQElV5ATL5XHMbaoZ7gfinOLpYWbQjmUkFeiQf7dRaRTsmvgVCXD7ohJWB-H4E-frTnUTc5dPiSWJJi=w480-h320-no

Kushoto: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes na Lawi Sijaona 1957

NB: Kuna mtu anatajwa kama rafiki ya Abdul Sykes nikimjulisha kama Mzanzibari. Wakati ule nilipokuwa naandika kitabu hiki hakutaka jina lake lijulikane. Hivi sasa yeye ni marehemu. Mtu huyu ni Ahmed Rashad Ali.

GgV1oId2QrUzdMWw0GInJNLhb2LjGow0WLYFtCgNIKLd7gYUvhApSK1Id18J8GMeu9h36fy3TjdpAp-uodp3Rdzj-irrpdr9xRZWXK3dXWW5dRc5Uv4rAZhSP-Z7jF8tONA_UU3cgRZS9o0mTXrpyOc0YfIMHkZSJZjcGSKQNUPimk31ZMoixNsIRkkIz2Oh60fjxDrSsvzLhTF9rvzlmSaQECKBS9boJ8zfqTnwuoxZqu2SkB9TAHn1WeKGUmt-8KXx1sd-U61ksGjoe568NMWkAwwEJtvOpeEus2PC39C08zdoDO5E7zaB9Q95QIgtI4AaxLBYWWy5GKKnKqWsUm_78jFhIOfiUwN29dU3dVJHaBqziXw0GFRBAfFzO10pMKv5ceCX2ID0G8CYBYauczPn54R-vE8R4I0pampJf3h43qLfS7slmOoLHhF7GJWDZwFEyQGmKGk9NrIrtbR74p6OBt9NqscMEjTihPmJM9akxImqvbKhi2DY0ar9bp5ScAODyFgrrvLViM9iaKHRQX1kdmRhUjOuZefRzLqMhlIBtCY7mX7vaI7XsYQlcZGXZLx2=w490-h690-no

Ahmed Rashad Ali

IMG-20160311-WA0114.jpg

Mpenzi msomaji ukipenda kusoma historia ya Ahmed Rashad Ali katika siasa za Afrika wakati wa ukombozi ingia hapa:

http://www.mohammedsaid.com/2013/12/ahmed-rashad-ali-bingwa-wa-propagand
 
Ahsante mzee wangu kwa historia hizi, Mungu akuongeze miaka tuzidi kufaidi........Naomba kuuluza huyu Abdul sykes ana uhusiano wowote na huyu muimba bongofleva Dully Sykes....
 
Isijekuwa umechanganya kati ya urafiki wa mtu na mtu na urafiki wa taifa kwa taifa!
Wise...
Najua unapata tabu...
Hii ndiyo kawaida ya historia hii.

Akili inakataa kukubali na kuamini.

In Shaa Allah nitaingia Maktaba nikiuletee kisa cha Ally Sykes
na Denis Phombeah walivyokamatwa Salisbury Sourthern
Rhodesia wakielekea Lusaka, Northern Rhodesia mkutanoni.

Hawa walikuwa viongozi wa harakati za uhuru Tanganyika.
 
Ahsante mzee wangu kwa historia hizi, Mungu akuongeze miaka tuzidi kufaidi........Naomba kuuluza huyu Abdul sykes ana uhusiano wowote na huyu muimba bongofleva Dully Sykes....
Xavia,
Amin.
Dully Sykes ni mjukuu wa Abdul Sykes.
 
Isijekuwa umechanganya kati ya urafiki wa mtu na mtu na urafiki wa taifa kwa taifa!
Wise...
Hebu soma hapo chini nilichoandika katika kitabu cha Abdul Sykes:
''Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini. Mwezi Agosti Kaunda akawa Katibu Mkuu wa ANC. Haukupita muda Kaunda akaanza kupeleka barua Nairobi, Dar es Salaam na Johannesburg akiitikia rai ya Kenya African Union na South African ANC kuwa ''Lusaka inapasa kuwa mahali pa kukutana wazalendo kutoka nchi zilizo Kusini mwa Sahara.íUjumbe wa watu watatu wa TAA ulialikwa na Katibu Mkuu wa African Congress ya Northern Rhodesia, Kenneth Kaunda, kuhudhuria mkutano wa Pan African Congress (ANC) mjini Lusaka. Mwezi wa Novemba Ally Sykes alipokea barua kutoka kwa Kaunda akimwalika kuhudhuria mkutano huo. Wakati ule ANC ilikuwa na manungíuniko kadhaa dhidi ya Waingereza na ilikuwa imeamua katika mapambano yake kutumia njia za amani ambayo katika barua ambayo Kaunda alimpelekea Ally Sykes aliielezea njia hizo za amani kama hivi, ‘’Hutashirikiana na mtu yoyote katika shauri lolote litakalokuwa na madhara kwa maslahi ya Waafrika.’’
 
Lakini mbona hii familia ya Sykes haipo katika uongozi wa nchi hii.....√√√
Xavia,
Nadhani mapenzi yao yamekuwa zaidi katika biashara kuliko siasa.

Maana hata wajukuu zao ukikutananao ukiwauliza watakuambia,''
Uncle nina kikampuni changu kidogo hapo mjini...''

Abdul Sykes nadhani ndiyo Mwafrika wa wa kwaza kuwa na petrol
station (Caltex) Dar es Salaam ya 1950s na siku hizo alikuwa katika
harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Angalia hii:
Mohamed Said: THE BUSINESS GENIUS OF PETER HORACE COLMORE AND ALLY KLEIST SYKES
 
Ahsante sana kwa mada nzuri mzee Mohamed Said√√√
 
kaka mo'd Said kunashida ya watu kujipendekeza,mtu anasema,ulianzishwa na baba wa taifa wakati hajui nani hasa aliuanzisha, njaa nayo ina sehemu yake.
 
Back
Top Bottom