Ally Mayai Tembele anaichokoza Yanga

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Na Ally Mayai Tembele

Niliwahi kuandika Yanga inajidanganya yenyewe na kuishi kwa kivuli cha timu kubwa na kudhani labda dunia imesimama kumbe dunia inakimbia kwa kasi mno.

Nilisema Yanga imedumaa na Siku ikija kushtuka na kutaka kwenda sambamba na dunia itakuta tayari Simba imeliteka soko lote la Uchumi wa soka nchini.

Nilitoa mfano wa Juventus, Porto, Buyen Munich, Mazembe, Gor na Horoya kwamba timu hizi tayari zimejimilikisha Uchumi wa soka wa nchi zao. Leo hakuna mchezaji wa Kijerumani asiyetamani kuchezea Buyern. Au mchezaji anayezaliwa Italy ndoto yake kuu ni kucheza Juventus.

Na tunakoelekea na Tanzania hali ndiko inakoelekea. Simba inajimilikisha kwa kasi ya ajabu uchumi wa soka.

Yanga wamebaki kujivunia juzi na jana na sio leo na kibaya zaidi sioni kesho yao. Kama Kuna kosa kubwa kuliko yote linafanyika ni pale wanapobeza mafanikio ya Simba na kuwaponda mwekezaji wa Muhamed Dewji.

Wamekuwa wakitafuta mapungufu machache yaliyopo Simba na kuyafanya ndio agenda yao. Wamesahau kabisa kuitazama timu yao na mkwamo uliopo wameamua kuitukuza Simba na kuitaja aidha kwa mapungufu au kuwabeza Kama watani. Wanasahau hapa wao wenyewe ndio wanaikuza brand ya Simba na kuifanya kutajwa mno midomoni kila siku.

Leo Yanga hawana hata Jambo Moja wanaloweza kupambana na Simba aidha ndani au nje ya Uwanja. Wamezidiwa kila idara na itawachukua muda mrefu mno kufikia Simba ilipo Sasa.

Yanga hawajakubali bado kubadilisha mfumo wao wa uendeshaji wa timu kutoka wa kizamani na wa kiholela kuja kwenye mfumo wa kisasa na hii inasababishwa na walaghai tena wezi wa jasho la wachezaji kuwahadaa ni timu ya wananchi na wasikubali mwekezaji kwa kuwa timu itakuwa si Mali yao tena. Huu ndio uongo uliotukuka wanaoutumia walaghai kuendelea kujinufaisha kupitia klabu hii.

Embu tujiulize nyie wapenzi na mashabiki wa Yanga lini mlinunuliwa hata soda na klabu zaidi ya nyie kuchangishwa? Sasa hicho mnachoaminishwa mtakipoteza ni kipi? Wanaoogopa kupoteza ni wale akina fulani ambao maisha yao yanategemea timu kuendelea kuishi mjini.

Na hawa huwa hawachangii zaidi ya kuwa mstari wa mbele kuhamasisha ili wazizungukie mlango wa nyuma wakaziibe. Sisi tunaochanga Wala hatuna Cha kupoteza

Nahisi kwenye miaka ya sitini ni kweli mashabiki wa Yanga labda walikuwa wengi kuliko wa Simba na mkabweteka na mkasahau watu wanazaliwa na kufa.

Nimebahatika kwenda karibu viwanja vyote vya soka nchini. Nawahakikishia kwa sasa Simba Ina mashabiki wengi kuliko timu zote nchini.

ENDELEENI KULALA MKIAMKA TAYARI JUA LITAKUWA LINAZAMA.
 
Mpira wa tanzania unashida sana, tena hawa wanaojiita wachambuzi.

Leo upepo ukienda vizuri msimbazi baasi yeye ataandika anayotakaa kuhusu yanga! Nashangaa hii makala ameandika ALLY MAYAY tunaemfahamu sisi. Kuona simba kashinda mechi mbili basi, kaona yanga bado imeng'ang'ania mfumo wa zamani. Hivi huyu Ally hajui yanga wako katikati ya mchakato wa mabadiliko?
 
Naona wewe unaijua vizuri Yanga kuliko huyo bwana!
 
Mchakato usioisha

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
 
Mashabiki wa Yanga tusimsikilize huyu Alli Mayayi amelipwa ili kuichafua na kuihujumu club yetu ya Yanga.

Na hiyo yote ni kwasababu alikuwa anataka uongozi ndani ya Yanga akakosa sasa ana hasira na Yanga ndo mana anatufanyia uhuni huu.
WITO KWA YANGA: tuendelee na uendeshaji huu huu wala tusiwaige Simba, Simba ile timu ni ya Mwamedi sasa. Sisi tuendelee kujiita timu ya wananchi na tuendelee kupost picha mitandaoni za wananchi tukiwa uwanjani kushabikia timu yetu.

Narudia tena, tuendelee na utaratibu huu huu wa uendeshaji wa timu yetu, tutafanikiwa muda siyo mrefu na Simba hawatatukuta

MwanaYanga mwenzangu VIMBAA VIMBAAA VIMBAA, na msimu huu kombe la ligi ni letu kwa kuwa tumemzidi Simba kwa mechi na points
 
Hahaa haaa bila shaka sindano imekuingia panapo. So tulia sasa dawa ifanye Nazi.
 
Yeye kasha fanya nini cha mfano watu waige au ni mboyoyo tu, anataka kusema Yanga ya sasa ni sawa na ile ya msimu miwili iliyopita?
 
Hizi ni propaganda za utelembwe tu wasimsingizie Ali, hivi mtu ukizunguka viwanja vyote nchini ndio kigezo cha kujua timu flani ina mashabiki kiasi gani? eti yanga labda ilikua na mashabiki wengi miaka ya sitini wakajisaau na kubweteka kwamba mashabiki wanakufa na kuzaliwa hii ni oja ya kijinga kabisa, kwa mahana hiyo wanaokufa ni mashabiki wa yanga pekee na wasimba hawafi? na wote wanaozaliwa ni mashabiki wa simba pekee?
Huyu atakua sio Ali Mayai na kama kweli ni yeye basi IQ yake ni ndogo Sana kwa vigezo vipi mpaka aseme yanga awawezi kushindana simba ndani na nje ya uwanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…