Ally Salim atemwa, Aishi Manula arejeshwa kikosini Taifa Stars

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mlinda mlango wa Simba SC Aishi Manula amejumuishwa katika kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza mechi za kuwania kufuzu CHAN 2025 baada ya kukaa nje ya kikosi hiko tangu Machi 2024

Tanzania itaikabili Sudan ugenini Octoba 27 2024 huku mechi ya marudiano itapigwa Benjamini Mkapa Novemba 3 2024.

Kikosi hiko chenye wachezaji 24 kitakuwa chini ya kocha Bakari Shime ambaye pia ni kocha mkuu wa timu za taifa za wanawake pia kimejumuisha wachezaji 11 kutoka katika kikosi cha Tanzania U20 ‘Ngorongoro Heroes’ ambacho kimetoka kubeba ubingwa wa CECAFA juzi Dar es Salaam.

1729600240592.png
 
Hilo jina la mwisho ni Crispin au Cyprian?
 
CHAN inaweza ikawa na kikosi chake tofauti na kile cha kushiriki mashindano mengine kama qualifiers za AFCON na WC
 
Kwangu nimeona kama ipo kwa ajili ya kuwajenga zaidi pia vijana ambao wataibeba stars pia hapo baadae bila kusahau mchanganyo wa wachezaji wazoefu hasa eneo la goalkeeping........na baadhi ya maeneo

So sitashangaa kwenye afcon qualifier akaitwa kama kawaida.,...

Au ngoja nianzishe Uzi....kwamba
Mudathir Yahya
Kibu Denis
Bakari nondo
Ibra Bacca
Tshabalala
Dickson job
WATEMWA STARS.....
 
Arudishe confidence.
Arudishe match fitness.
Arudishe ubora wake.
Kwenye afcon qualifiers akae kwenye milingoti mitatu.
 
Kwangu nimeona kama ipo kwa ajili ya kuwajenga zaidi pia vijana ambao wataibeba stars pia hapo baadae bila kusahau mchanganyo wa wachezaji wazoefu hasa eneo la goalkeeping........na baadhi ya maeneo

So sitashangaa kwenye afcon qualifier akaitwa kama kawaida.,...

Au ngoja nianzishe Uzi....kwamba
Mudathir Yahya
Kibu Denis
Bakari nondo
Ibra Bacca
Tshabalala
Dickson job
WATEMWA STARS.....
Haha 😂
aisee kweli wababe wametemwa, muda wote namtafuta Baka na Nondo siwaoni!
 
Manula ni garasha
Huo ni mwanzo wa kufeli kwa Tanzania sijui ni nani huwa ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho kwenye mambo ya nchi hii
 
Yaweza kuwa makosa ya kukusudia....hapo fuatilia umri wa huyo Crispin, atakuwa mkubwa kwa Cyprian Ngushi😀😀😀
 
Back
Top Bottom