Ally Sykes katunukiwa barabara

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ALLY SYKES KATUNUKIWA BARABARA

Rafiki yangu mmoja hapa FB kaniletea ujumbe jana usiku akinifahamisha kuwa kaona kibao cha Ally Sykes alichotunikiwa katika barabara mojawapo jijini Dar es Salaam.

Mimi nikiwa na fikra ya kibao ambacho Ally Sykes alijipa mwenyewe mtaani kwake Mbezi Beach nikamwambia huyu sahib yangu kuwa apige picha hicho kibao kisha anirushie ili mimi nimpe historia ya kibao hicho.

Leo nimepokea picha mbili za kibao chenye jina la Ally Sykes nami nikawa nimeshangaa.

Kwanza kilichonishangaza ni kibao chenyewe sicho hicho nilichokuwa nakijua mimi na wengi wakazi wa Mbezi Beach wanakifahamu.

Ndugu yangu kaniandikia ananiambia kuwa kibao hicho kipo Tangi Bovu.

Katika miaka ya 1980 wakati Kitwana Kondo alipokuwa Meya wa Jiji alitoa baadhi ya majina ya mitaa ya Dar es Salaam akawatunuku wapigania uhuru waliokuwa TANU kama Tatu bint Mzee, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Julius Nyerere, John Rupia, Bi Khadija Kamba na wengineo.

Kleist Sykes baba yao Abdul, Ally na Abbas na yeye akapewa Mtaa wa Kipata, mtaa ambao aliishi.

Ingawa yeye hakuwa katika TANU lakini anafahamika kama muasisi wa African Association 1929 na anafahamika kwa sifa nyingi katika mji wa Dar es Salaam.

Wakati wa Dar es Salaam Municipal Council Kleist alikuwa Mwafrika wa pii kuwa katika bodi ya Municipal.

Mwafrika wa kwanza alikuwa Juma Mwindadi.

Ally Sykes yeye hakusubiri City Council ikaweke kibao Mtaa wa Kipata chenye jina la baba yake.

Ally Sykes alitengeneza vibao vyake mwenyewe na vibao hivi akaviweka Mtaa wa Kipata.

Ally Sykes akaweka pia vibao vyenye jina lake Mbezi Beach katika barabara ya mchanga inayokwenda nyumbani kwake.

Meya Kitwana Kondo akapata taaarifa kuwa Ally Sykes kajipa mwenyewe kibao chenye jina lake katika mtaa wa nyumbani kwake.

Mzee Kondo kwa kumjua Ally Sykes na bila shaka kwa kutambua kuwa anastahili kuadhimishwa alinyamaza kimya hakusema lolote.

Alicheka na kutingisha kichwa akijiambia, ''Huyo ndiye ndugu yangu mie Ally Sykes.''

Angelitaka Kitwana Kondo angeweza kuwatuma wafanyakazi wa Jiji wakaving'oe vibao vile.

Mzee Kondo hakufanya hilo.

Hili jambo likawa kama vile limekamilika na wote wawili hakuna aliyelisemea hili jambo hadi wote wanaingia kaburini.

Alitangulia Ally Sykes na Kitwana Kondo akamfuata.



Katika mziko ya hawa baba zangu kote nilisimamishwa kuzungumza mchango wao katika historia ya Tanganyika.

Kuna watu hawakupedezewa kuona majina ya mitaa yamebadilishwa kwa kuwaenzi hawa wapigania uhuru wa Tanganyika.

Kilichokuwa kinawaunguza nyoyo ni kuwa majina yote ukiondoa la John Rupia na Julius Nyerere yalikuwa majina ya Kiislam.

Mzee Kondo akafanyiwa mahojiano na Sarah Dumba wa TBC kuhusu kubadilisha majina ya mitaa.

Magazeti yote yalikuja juu sana wakamshambulia Mzee Kondo kuwa amefanya yale kwa sababu ya udini.

Mzee Kondo akawajibu akasema ikiwa nyie hamjui hawa watu walifanya nini katika nchi hii ulizeni mtaelezwa.

Mtaa wa Tandamti ambao ulibadilishwa jina na kuwa Mshume Kiyate hadi leo wenye mamlaka wamekataa kubadilisha kibao sasa yapata zaidi ya miaka 30.

Kuwa sasa Ally Sykes katunukiwa barabara hili ni jambo zuri sana.

Ally Sykes alighadhibika sana Yusuf Makamba alipopewa mtaa Gerezani.

Ally Sykes akawa anasema, ''Hawa watu wabaya sana wanaacha kumpa Dossa Aziz mtaa Gerezani wanakwenda kumpa Yusuf Makamba?

Kwa lipi kubwa alilofanya Makamba kumshinda Dossa?''
 
Leo ndio nimejuwa usahihi wa jina siyo Max Mbwana bali Makisi Mbwana.
 
Matola,
Makisi ni jina la Kizaramo.

Lakini jina hili likawa linaandikwa "Max.''
Hapo ndipo lilipotokea tatizo.

Mzee Makisi Mbwana alikuwa kiongozi wa Uzaramo Union.
 
Mzee wangu pale uliposema kuwa "John Rupia na Julius Nyerere ndio Wakristo wawili tu" ulidhamiria kufikisha ujumbr gani?

Andiko lako zuri ila unalitia dosari.

Anyway kundi lote liliongozwa na Julius hadi kupata Uhuru.
 
Mzee wangu pale uliposema kuwa "John Rupia na Julius Nyerere ndio Wakristo wawili tu" ulidhamiria kufikisha ujumbr gani?

Andiko lako zuri ila unalitia dosari.

Anyway kundi lote liliongozwa na Julius hadi kupata Uhuru.
Einstein...
Nyerere katika hotuba yake ya muago Diamond Jubilee Hall mwaka wa 1985 alisema kuwa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika yeye alizungukwa na Waislam Wakristo walikuwa wawili yeye na Rupia.

Mimi sikuwa na ujumbe wote ila kueleza historia ya uhuru ilivyokuwa.

Ama kuwa Nyerere alikuwa kiongozi hakika alikuwa kiongozi wa TANU na harakati za uhuru lakini peke yake bila ya kuungwa mkono na hao aliiwataja Ukumbi wa Diamond asingepata hata huo uongozi wa kuwa Rais wa TANU 1954.

Kuwataja Waislam ndiyo imekuwa dosari?
Kwani wewe huijui historia ya uhuru?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…