Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Haya nimeyatoa katika mswada wa kitabu nilichoandika na Ally Sykes ''Under the Shadow of British Colonialism,'' yapata miaka 20 iliyopita.
Ananihadithia safari yake ya kwenda Accra, Ghana mwaka wa 1957 kuhudhuria sherehe za uhuru wa Ghana chini ya Kwame Nkrumah. Safari hii alifanya kwa barabara kutoka Dar es Salaam hadi Accra.
Safari zake zote kuanzia safari ya kwenda Mozambique (1952) kuona kijiji alichotoka babu yake, Sykes Mbuwane, Rhodesia (1953)alikokua anapita njia kwenda kuhudhuria mkutano wa wapigania uhuru Kusini ya Sahara ulioitishwa na Kenneth David Kaunda, Nyasaland alikopita na Denis Phombeah wakiwa wajumbe wa TAA Ally Sykes alikuwa akisafiri na pasi ya Kireno kama Mzulu.
Katika safari yao hii Ally Sykes na Dennis Phombeah wakisafiri kama wajumbe wa TAA walikamatwa Salisbury, Rhodesia na kufukuzwa. Kufukuzwa kwao ndiyo sababu ya yeye kufika Nyasaland kwao Denis Phombeah wakiwa njiani kurejea Tanganyika.
Ally Sykes anasema alipofika Leopoldville, Belgian Congo alipanga kwenye nyumba ya kulala wageni katika ya mji karibu na soko. Anasema ilikuwa hapo ndipo alipoona kwa jicho lake mwenyewe Wabelgiji wakiwapiga viboko Wakongomani.
Jambo hili lilimuuma sana kwani Wabelgiji kwa kitendo kile walikuwa wamewageuza Waafrika kama wanyama ambao wanaweza wakaswagwa na viboko.
Kutokea hapo Leopoldville akavuka mto na kuingia Congo Brazzaville upande wa pili wa mto. AIly Sykes akaingia Lome, Togo na kutoka hapo akaingia to Accra, Ghana. Safari yote kutoka Dar es Salaam hadi Accra ilimchukua siku 18. Ally Sykes anasema nchi zote hizo alizopita hakuona ushenzi kama ule alioshuhudia Leopoldville wa Mwafrika kucharazwa viboko hadharani watu wakishuhudia.
Picha: Dennis Phombeah na Ally Sykes na Julius Nyerere 1958.