Alosema kiswahili hakiwezi kuwa lugha ya kitaalamu ni alikosea

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Wapo wanaoamini eti kuna maneno au vitu vya kitaalamu ambavyo kwa kiswahili havina maana.
kwanza hao ni wale wavivu sana wa kufikiri,kujifunza na kuwaza.
jiulize je 'television' ilikuwepo kabla ya kiswahili au baada ya kiswahili ?
kwanini leo ikaitwa 'runinga' .
tazama kitu car ambalo liliitwa gari au *website* ambayo ikaitwa 'tovuti' .
je nani alivipa majina ya kiswahili .
Kuna uvivu unafanyika hasa wa wataalamu wa kiswahili katika kukifunza kiswahili.
 
Mkuu unaonekana ni mdau namba moja wa Kiswahili hapa jukwaani!!

Kama ni hivyo nadhani unaweza kuwa na mahusiano ya karibu na Baraza LA Kiswahili. Naomba unifikishie ujumbe wangu kwao kuwa
Wamelala sana, nimesaka tovuti yao sioni popote ilipo! Nikajaribu Baraza la Kiswahili Zanzibar pia hola!! Nikajaribu TATAKI napo nimeambulia patupu!! Taasisi zinazohusika na usimamizi na ukuzaji wa kiswahili hazina hata tovuti ni aibu!!!
 
We ndo utakuwa mwendawazimu!Kwa nini ulazimishe watu wajifunze kiswahili na si kisukuma?Mtu anazaliwa hajui kiswahili wala kiingereza,anaingia shule ya msingi ndo anaanza kujifunza kiswahili,akiingia sekondari anajifunza kiingereza,lakini ukimuuliza density ni nini kwa kiswahili haifahamu,inaonekana kupata maarifa kwa kiingereza ni rahisi kuliko hicho kiswahili chako.
Halafu hii kampeni ya kiswahili inaniboa sana maana inawaangukia watoto wa maskini tu huku matajiri wakijifunza kiingereza na ndio wanakuja kututawala.
 
Kukosekana huko kwa tovuti pia kunatufanya watafiti tunaotamani kufanya tafiti kwenye Kiswahili kukosa mahali pa kuanzia kupata habari, changamoto, "resources" za Kiswahili nk.

Mfano, hadi sasa hakuna resources kama vile "corpus" ambayo iko chini ya hizo taasisi! Zipo zinazomilikiwa na vyuo kama Helsinki na za wakenya Kama vile Sawa corpus!!

Bado viongozi wa taasisi kama hizi wanalalamika pale wakenya wanapopewa nafasi za project kwenye makampuni kama Google na Microsoft kwa ajili ya uandaaji na tafiti kwenye Kiswahili.

Wakumbushe waamke
 
We ndo utakuwa mwendawazimu!Kwa nini ulazimishe watu wajifunze kiswahili na si kisukuma?Mtu anazaliwa hajui kiswahili wala kiingereza,anaingia shule ya msingi ndo anaanza kujifunza kiswahili,akiingia sekondari anajifunza kiingereza,lakini ukimuuliza density ni nini kwa kiswahili haifahamu,inaonekana kupata maarifa kwa kiingereza ni rahisi kuliko hicho kiswahili chako.
Halafu hii kampeni ya kiswahili inaniboa sana maana inawaangukia watoto wa maskini tu huku matajiri wakijifunza kiingereza na ndio wanakuja kututawala.
Nakubaliana na wewe mahali!!! Kuna sehemu sera yetu ya Elimu umekosa kugusa panapotakiwa, ndo maana tumebaki kutapatapa tu, kiswahili tunachojua ni cha mtaani tu wala siyo cha kitaaluma!! Kingereza ndo basi tena!!

Kwanini? "timing" kama tunaamua kukomaa na kingereza, basi kianzie darasa LA kwanza kwa Masomo yote. Akili ya mtoto inapokuwa changa inakuwa na uwezo mkubwa sana wa kujifunza. Kumwanzishia mtu kingereza sekondari, ilihali ulimi ulishapinda ni kumuonea!! Ndio maana matokeo yake tunavurunda sasa, maana misingi ya Kiswahili tunaiacha shule ya msingi!! Kingereza nacho tunakikutia "uzeeni" tunakosa "competence" kila mahali
 
Unania njema sana na taifa lako lakn kimantik unataka kuliangamiza taifa lako unazalisha nn ili uitie nguvu kiswahil kisomwe na watu wengi unconstitutional??
Kupumbuka mambo haya hatutumii nguvu bal n akil tu, na kama unataka kunijbu unijbu kiakil zaid
 
Nimependa swali lako sana,NAZALISHA NINI ILI KUTIA NGUVU KISWAHILI ?
ingia katika google halafu andika neno -MIMI MALENGA- tafuta hadi uone nembo yenye nusu jua na kitabu na chini maneno ya -MIMI MALENGA- kisha fungua hapo.
**KUNA VITU SHERIA ZA JF HAVITURUHUSU KUWEKA HAPA.
 
Umenipa kazi sawa ntaifanya lakn na ww pia ukakipitie vzur je tunazalisha vtu vifuatavyo vpo??
Electrical equipments
Laboratory tools
.
.
.
.
 
Mkuu unaonekana ni mdau namba moja wa Kiswahili hapa jukwaani!!

Kama ni hivyo nadhani unaweza kuwa na mahusiano ya karibu na Baraza LA Kiswahili. Naomba unifikishie ujumbe wangu kwao kuwa
Wamelala sana, nimesaka tovuti yao sioni popote ilipo! Nikajaribu Baraza la Kiswahili Zanzibar pia hola!! Nikajaribu TATAKI napo nimeambulia patupu!! Taasisi zinazohusika na usimamizi na ukuzaji wa kiswahili hazina hata tovuti ni aibu!!!
Check hapa mkuu: Baraza La Kiswahili la Taifa - BAKITA
 
Wapo wanaoamini eti kuna maneno au vitu vya kitaalamu ambavyo kwa kiswahili havina maana.
kwanza hao ni wale wavivu sana wa kufikiri,kujifunza na kuwaza.
jiulize je 'television' ilikuwepo kabla ya kiswahili au baada ya kiswahili ?
kwanini leo ikaitwa 'runinga' .
tazama kitu car ambalo liliitwa gari au *website* ambayo ikaitwa 'tovuti' .
je nani alivipa majina ya kiswahili .
Kuna uvivu unafanyika hasa wa wataalamu wa kiswahili katika kukifunza kiswahili.
SIKUAMINI LAKINI NAENDELEA KUJIFUNZA.
KATIKA"Oxford Advanced Learner's Dictionary",
International Student's Edition
Eighth edition
iliyochapishwa na Oxford University Press (2010)
Nimekutana na maneno ya Kiswahili katika kurasa zake mbalimbali.
Ukiperuzi Dictionary hiyo Alphabetically, na kwa namna yalivyopewa tafsiri ni kusema hayo sasa ni maneno Mzungumzaji wa Kiingereza anaweza kuyatumia wakati akiongea Kiingereza..
baadhi yake ni haya:-
mama, baba, mzee, mwalimu, safari, kanzu, khanga
SIKUAMINI.
Naendelea kujifunza.
 
Shida inakuja pale ambapo sisi wenyewe hatutaki kukithamini kiswahili.
 
Mkuu unaonekana ni mdau namba moja wa Kiswahili hapa jukwaani!!

Kama ni hivyo nadhani unaweza kuwa na mahusiano ya karibu na Baraza LA Kiswahili. Naomba unifikishie ujumbe wangu kwao kuwa
Wamelala sana, nimesaka tovuti yao sioni popote ilipo! Nikajaribu Baraza la Kiswahili Zanzibar pia hola!! Nikajaribu TATAKI napo nimeambulia patupu!! Taasisi zinazohusika na usimamizi na ukuzaji wa kiswahili hazina hata tovuti ni aibu!!!

Tovuti ya BAKITA ni hii>>>>> Baraza La Kiswahili la Taifa - BAKITA
 
Back
Top Bottom