Tusker Bariiiidi
JF-Expert Member
- Jul 3, 2007
- 5,551
- 2,153
Nikiwa mteja wa muda mrefu wa Alpha Dry cleaner,nilifurahia sana kitendo cha kwao kutuletea/kutusogezea huduma karibu kwa kufungua duka /Outlet mpya Mlimani City Mall na kama mnavyofahamu karibu huduma zote zinazopatikana hapo karibu asilimia 97 zinafunguliwa siku zote saba za wiki mfano ni benki za NBC,NMB,CRDB,TWIGA na EXIM pia maduka ya kampuni za simu kama ZAIN,TIGO na VODACOM yanatoa huduma zake siku zote iwe sikukuu au wikiendi lakini mimi nimesikitishwa na kitendo chao Alpha Dry Cleaner kufungua duka lao mfano kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni kwa siku za wiki na jumamosi saa 3 asubuhi mpaka saa 9 mchana!! na kufungwa siku za Jumapili na siku za sikukuu!!! sasa mimi sijaelewa umuhimu wa wao kuleta duka hilo hapo Mlimani city na kujaza eneo ambalo lingeweza kuongeza ufanisi wa kupatikana huduma nyingine ambazo zinamfanya mteja azifuate katikati ya jiji. Tafadhali uongozi wa Alpha Dry Cleaner uliangalie hilo... NAWASILISHA!!