1. Ubora wa engine.
Alphard inakuja na 2AZ na 1MZ wakati Brevis inakuja na 1jz fse au 2jz fse.
2AZ ina majanga yake ya kula Oil kama inakunywa maji baada ya muda fulani.
1mz ni engine nzuri ila ni Cc2996
1jz fse na 2jz fse ni engines nzuri ila hazitaki ujanja ujanja otherwise Brevis utaichukia.
2. Matumizi ya mafuta hata hazitofautiani, nenda na yoyote.
3. Spea zipo Bwerere ila Master Cylinder ya Brevis inashare na Land Cruiser 100 series bei mkasi usije sema hatukukuambia.
4. brevis inaweza kustahimili mazingira ya vijijini. Alphard iko chini sana.
Japo hizi gari hazifanani kabisa sijui umewaza nini kuzilinganisha.,