JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Huyu ni mojawapo ya Binadamu niliopata kuwafuatilia kidogo, tangu niliposikia jina lake lilitajwa kuwa amepewa dhamana Nchini. Hebu Tazama; 👇🏾👇🏾
DISEMBA 2015
- Aliteuliwa kuwa KAIMU Kamishna Mkuu TRA akitokea nafasi ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi aliyoitumikia tangu Agosti 2013.
MACHI 2016
(Takribani Miezi mitatu hivi)
Akathibitishwa rasmi kuwa KAMISHNA MKUU - TRA.
(Mwaka Mmoja baadae)MACHI 23, 2017
-Akateuliwa kuwa Katibu Mkuu, IKULU.
- Akateuliwa kuwa BALOZI huku akisubiri Uapisho na kupangikiwa kituo cha Kazi.JANUARI 11, 2018
MEl 20, 2018
-Akaapishwa kuwa BALOZI wa Tanzania Nchini CANADA.
- Uteuzi wake Ukatenguliwa, na akaondolewa “HADHI” ya Ubalozi na akarudishwa Nchini.NOVEMBA 8, 2018
Siku kadhaa baada ya “kutenguliwa” Ubalozi na kurudishwa Nchini, Novemba 2018 Gazeti Jamhuri liliandika Stori kwamaba anatarajiwa kufikishwa MAHAKAMANI kujibu tuhuma kadhaa (TRA).!
Lakini hakufikishwa Kortini.
SEPTEMBA 2019
- Akateuliwa tena kuwa RAS (Katibu Tawala), Mkoa wa Mtwara.
- Mhe. Rais Samia S. Hassan akamteua tena kuwa KAMISHNA Mkuu - TRA.!APRILI 4, 2021
JULAI 2, 2024
- Kidata, baada ya kutumikia nafasi hiyo kwa mara ya Pili. Wakati huu akiwa amekaa Ofisini SIKU 1,185 ( Mishara ya takribani Miezi 39 ),sasa anafungasha TRA na kuelekea Ikulu baada ya kuteuliwa kuwa MSHAURI WA RAIS - IKULU.
Andiko la: Stanslaus Lambat