Mwanariadha wa kimataifa, atakaeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Olimpiki Japan mwaka huu Alphonce Felix Simbu ameshinda mbio za BIMA Marathon 21K kwa muda wa (1:02:09), naye mwakilishi pekee wa kike wa mashindano ya Olimpiki Failuna Abdi Matanga ameshinda mbio hizo kwa muda wa (1:16:52)
Katika mbio hizi, wao wamekimbia ili kujipima miili yao na Maandalizi ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo Japan August 8, 2021 (kwa Marathon).