Wewe mpuzi kweli
Unakimbilia kwajirani wakati ndani ya nyumbayako nako kunamoto
Jana kuna Wanaume walifanya yao kenya mbona umechuna!!!
Mwanamke auawa, 3 wajeruhiwa na Al Shabaab Mandera
MWANAMKE aliuawa kwa kupigwa risasi huku watu wengine watatu wakijeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na wafuasi wa kundi la kigaidi la Al Shabaab katika miji ya Lafey na Mandera.
Shambulio hilo, lililotekelezwa mwendo wa saa moja na nusu Jumamosi, lililenga abiria waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja kutoka mji wa Mandera wakielekea kuhudhuria hafla ya mazishi mjini Lafey.
Akiongea na wanahabari kwa njia ya simu, naibu kamishna wa Lafey Erick Ornyi alisema wanamgambo hao wapatao 20 waliokuwa na silaha hatari walichomoka kutoka msituni na kulimiminia risasi gari hilo.
Afisa huyo alisema dereva wa gari hilo alilisimamisha baada ya kupigwa risasi mguuni na mkononi.
Ornyi alisema washambuliaji hao walitoweka na mali ya waathiriwa hao wakielekea nchini Somalia.
Bw Ornyi alisema maafisa wa usalama walitumwa eneo la tukio lakini hadi kufikia jana walikuwa hawajawakamata washambuliaji hao. Waliojeruhiwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mandera.
Bunduki 15
Shambulio hilo lilitokea saa chache baada ya wafuasi wa Al Shabaab waliokuwa na silaha kushambulia kituo cha polisi cha Diff katika kaunti jirani ya Wajir. Walitoweka na bunduki 15 na risasi kadha.
Kufuatia msururu wa mashambulio ya Al Shabaab eneo hilo, Gavana wa Mandera Ali Roba ametoa wito kwa Serikali ya Kitaifa kupeleka Polisi wa Akiba 900 eneo hilo.
Barabara kutoka Lafey kwenda Wajir ilifungwa na Serikali mnamo Desemba 2014 baada ya wanamgambo wa Al Shabaab kuwaua raia 28 waliokuwa wakisafiri kwenda Nairobi. Wengi wao walikuwa walimu waliokuwa wakienda manyumbani kwa likizo ya mwisho wa mwaka.
Maafisa wa usalama wa eneo hilo sasa wanawashauri wenye magari, hasa ya uchukuzi, kutumia barabara ya Rhamu kwenda Wajir ambayo iko mbali na mpaka wa Somalia.
Wakati huo huo, mabasi ya uchukuzi wa abiria kutoka Mandera yamesitisha safari za kwenda Nairobi katika kipindi cha wiki moja iliyopita wasimamizi wakihofia hali mbaya ya usalama katika kaunti ndogo ya Elwak. Mashambulio kadha ya kigaidi yamekuwa yakishuhudiwa katika eneo hili.