Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
ALTEZZA TRAVEL MLIPA KODI BORA WILAYA YA HAI K'NJARO
MOSSHI
Kampuni ya wakala wa Utalii ya Altezza Travel imeshinda Tuzo ya mlipa Kodi bora kwa walipa Kodi kutoka wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro .
Tuzo hizo zimetolewa wiki iliyopita Katika hafla fuoi ya kutunuku Tuzo kwa walipakodi bora iliyoandaliwa n'a mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)mkoani Kilimanjaro na kufanyika kwenye ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.
Kampuni ya Altezza moja ya Kampuni kubwa za wakala wa Utalii imekuwa ikifanya vizuri katika ulipaji wa Kodi za serikali.
Tuzo hiyo ilipokelewa na meneja wa Kampuni hiyo,Dickson Muganda ambaye baada ya Tuzo hiyo alizungumza na waandishi wa Habari .
Alizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jengo la NSSF COMPLEX, Muganda amesema kuwa Tuzo hiyo ni heshima kwao na ni kielelezo cha kuongezeka kwa watalii.
Alisema wao kama ALTEZZA wanaahidi kuendelea kuiuza Tanzania ili ongezeko hilo la wageni liendelee kuongezeka.
Alisema ongezeko hilo pia litachangia kuwepo na ongezeko la Mapato yanayotokana na sekta ya Utalii.
Kulingana na meneja huyo,ongezeko la Watalii pia limechangiwa na kampeni kubwa iliyofanywa na mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia filamu yake ya Royal Tour.
Alisema Tuzo hiyo pia inawapa nguvu ya kuwekeza zaidi na kuona wanatoa huduma bora kwa wageni pamoja na kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi wao wakiwamo wapagazi,waongozaji wageni na wapishi hiii ni kwa eneo la wageni wanapanda . mlima Kilimanjaro .
Hata hivyo alisema kampuni hiyo iliteteleka kidogo na kushindwa kupata Tuzo kwa miaka miwili kutokana na kuyumba kwa soko lao kutokana na vita vinavyoendelea Kati ya majeshi ya Urusi na Ukraine
Mwisho