Gari zote nimetumia
Analysis;
1) Altezza
- Ni gari nzuri sana na ngumu kwelikweli, inadumu sana. Ndio maana ipo kwenye kundi la sports car.
- Inabwia wese, Altezza zipo za aina mbili Altezza(sedan), Altezza Gita(station wagon) na katika hzo alteza zipo za4cylinder na 6cylinder.
- Kwa urban trips, litre moja inakwenda km 8-9, usiongopewe na mtu yoyote huo ndio wastan na ikitumika sana kwa miaka kadhaa wastan hushuka hadi litre 1 kwa km 7-8.
- kwa safari ndefu, 4cylinder inakwenda hadi km kati ya 12-15 kutegemeana na ubora wa gari yako.
- kama shuguli zako ni tripu za mjini tu, sikushauri kwa maana itakufilisi wese.
- Thamani yake kwa sasa ime-drop sana, hata ukiamua kuja kuiuza utaiuza kwa bei ya hasara
2)Premio
- Ni gari nzuri sana, kibongobongo tunasema zipo old model na new model but wataalamu wanaziweka kwenye Generations kwa maana ss tunayoiita new model wala sio new model ni second generation( 2003 - 2007), new model zipo za mwaka(2007 - present).
- Kwenye hzo generations zake zipo za cc1490, cc1790 na cc1990. ushauri wangu nunua hzo za kati ya 2003 - 2007 zenye cc1490(1.5l) kwa urban trips zinakwenda litre 1 kwa km 10-13 kutegemeana na condition ya gari.
- Thamani yake kwa sasa ni kubwa sana, namaanisha watu wanavyozi-rate hata ukiamua kuja kuiuza utaiuza kwa pesa nzur tu.
3)Runx/Allex
- Ni gari nzuri sana, zipo comfortable lakini huwez linganisha na premio.
- Ni ngumu sana na zinadumu, ila tatizo nyepesi sana(1090kg).
- Zipo kuanzia mwaka 2001 - 2006, na zipo za cc1490 na cc1790.
- Kwa ushauri wangu nunua za cc1490.
- fuel consumption kwa urban trips ni litre 1 kwa km 10 - 14 kutegemeana na condition ya gari.
- kwa safari ndefu inakwenda litre 1 kwa km 12- 16 kutegemeana na hali ya gari.
- Watu wanazi-rate high sana, zina thaman kubwa sana. ukija kuiuza utaiuza kwa pesa nzuri
Hitimisho;
- Kwa gari zote hzo hapo juu, kama kipato kinaruhusu nunua premio ya 2016, ila kama kipato hakiruhusu nunua runx au allex hutojuta! kuhusu suala la spare, hzo zote hapo bei zake ni chee tu kasoro premio za 2016.