m_kishuri
JF-Expert Member
- Jan 27, 2010
- 1,484
- 372
WADAU, katika pilikapilika za maisha, nimemefanyikiwa kupita kwenye University ya MACMASTER (ON-Canada). Kwenye Library yao ya Health Science nimekutana na kibao chenye ujumbe ufuatao:
THE CLASS OF MEDICINE 1999 HAS PLEDGED THEIR SUPPORT TO THE HEALTH SCIENCES LIBRARY OF MACMASTER UNIVERSITY.
"MAY THIS GIFT FURTHER THE EDUCATION OF STUDENTS AT MACMASTER FOR YEARS TO COME AND INSPIRE THEM TO SUPPORT THEIR UNIVERSITY."
Ujumbe huu umenifanya nijiulize maswali kadhaa kuhusu mchango wa wanajamii wenzangu kwenye shule na vyuo tulivyopitia katika maisha yetu, haswa vyuo kama Mlimani, Sokoine, Mzumbe, n.k. Na hii haswa inatokana na sababu kwamba inapotokea mtu akakisema vibaya chuo fulani, mfano Mlimani au Sokoine, basi malumbano yanakuwa makali. Lakini swali ni je, unatoa mchango gani kuboresha hali ya wadogo zako uliowaacha pale. Kwa msisitizo zaidi, kama alivyosema Mr. Jay Naidoo, the former minister in Mandela first Gov. katika hutuba zake kwamba, Are you going to fit in or change the situation?
Watanzania wengi, ikiwemo humu jamvini ni wepesi kulalamika kuhusu kuanguka kwa hali ya elimu nchini, lakini nadhani ni wachache sana ambao wanafanya mambo kwa vitendo ili kurekeisha hali hiyo. Mchango wako (kwa kiasi uwezacho kwenye shule yako ya zamani) unaweza ukawa chachu kubwa ya maendeleo ya elimu nchini.
Ntakubaliana na wengi kuhusu suala la rushwa na matatizo mengineyo ya uzembe, lakini TECHNOLOGY imeturahisishia mambo kuliko hapo awali. Hivi je, MAALUMNI watano wa darasa la 1995 kutoka Faculty ya engineering pale mlimani hawawezi kujitolea kununua vitabu kadhaa, au kulipia online journals na publications ili ziweze kuwasaidia wenzao katika research zao? Au hata kubadilisha zile printer na computer wanazotumia wadogo zako kwenye ile faculty yako ya zamani, je hili haliwezekani?
Kwa wale ambao tayari wanafanya haya, natoa hongera na shukrani za dhati. Lakini kwa wale ambao tunakalia kulalamika tu kuhusu kushuka kwa ELIMU Tanzania, si vibaya kama tukiamua ku-change the situation badala ya kufit in.
http://hotbuzznews.net/role-of-alumni-in-higher-education/